Mwana wa
Rais Yoweri Museveni, Meja Jenerali Muhoozi Kainerugaba na mkewe
Charlotte Kutesa Kainerugaba alipokuwa anapandishwa cheo kuwa meja
jenerali Mei 25, 2016.
Rais wa
Uganda Yoweri Museveni amemteua mwanawe Meja Jenerali Muhoozi
Kainerugaba, kuwa mshauri mkuu wa rais kuhusu operesheni maalum.Mke wa
Museveni, Bi Janet Kataaha Museveni ni Waziri wa Elimu na Michezo,
wadhifa ambao alikabidhiwa Juni mwaka jana.
Jenerali
Kainerugaba amekuwa kamanda wa kikosi maalum cha wanajeshi (SFC) chenye
jukumu la kutekeleza operesheni maalum za kijeshi.Kikosi hicho husimamia
ulinzi wa rais na kulinda maeneo muhimu kwa serikali Uganda.Luteni
kanali Don Nabaasa amepandishwa cheo na kuwa kanali na akateuliwa kaimu
kamanda wa SFC.Rais Museveni pia amemteua mkuu mpya wa majeshi, Meja
Jenerali David Muhoozi ambaye amepandishwa cheo na kuwa jenerali.
Mkuu wa majeshi wa awali, Jenerali Edward Katumba Wamala amehamishwa na kuteuliwa waziri wa ujenzi.
Meja Jenerali Muhoozi Kainerugaba (kati) amekuwa kamanda wa kikosi maalum UgandaKwenye mabadiliko hayo yaliyotangazwa na msemaji wa Majeshi ya Ulinzi ya Uganda (UPDF)Luteni
Kanali, Rais Museveni amempandisha afisa mkuu wa majeshi aliyeongoza
operesheni ya kushambulia ikulu ya mfalme wa Rwenzururu, magharibi mwa
nchi hiyo.
Watu 100 walifariki wakati wa operesheni hiyo. Mfalme wa Rwenzururu Charles Wesley Mumbere alikamatwa na bado anazuiliwa
Brigidia
Peter Elwelu, aliyekuwa mkuu wa kikosi cha wanajeshi hao wenye kambi yao
kuu Mbarara, amepandishwa cheo na kuwa meja jenerali na akateuliwa
kamanda wa majeshi ya nchi kavu.
No comments:
Post a Comment