Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akizindua Jiwe la
Msingi la Kiwanda Keds.kwakushirikina na Mkurugenzi wa Kiwanda hiko, Jack
Feng.
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage ameweka jiwe la
msingi kuashiria kuanza kwa ujenzi wa Kiwanda cha Sabuni (Keds)
kilichopo Kibaha Mkoani Pwani.
Kiwanda hicho ni cha pili kujengwa katika Bara la Afrika baada ya cha kwanza kujengwa nchini Ghana.
Akizungumza
wakati wa uwekaji wa jiwe hilo,Waziri Mwijage amesema kuwa amefurahi
kuona mapambano yakuendeleza Tanzania ya Viwanda,amesema kupitia ujenzi
wa Viwanda hivyo ukuaji wa Uchumi utakuwa sambamba na ukuaji wa
Maendeleo ya Watu.
Pia
amesema kuwa Kiwanda hiko cha Keds kimeitoa Tanzania kimasomaso katika
kutimiza asilimia 40 ya upatikanaji wa ajira pamoja na kuziomba Mamlaka
za Mikoa kote nchini kuiga Mfano wa Pwani katika Uwekezaji wa Viwanda na
kujifunza ukarimu kwa wawekezaji.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini
(TIC),Clifford Tandari amesema kuwa ni fursa muhimu kwa kuwa Kampuni
hiyo tayari ina Kiwanda Ghana hivyo kujengwa Tanzania kitakuwa cha
pili.
Amesema kuwa baada ya Kiwanda hicho kuisha kitaokoa gharama za uingizaji wa sabuni kutoka nje.
Naye
Mkurugenzi wa Kiwanda hiko, Jack Feng,amesema tangu kuanza kwa mradi
huo wametumia muda mfupi kuweka sawa ardhi ya eneo hilo pia amesema kuwa
watajenga kwa uzoefu na ujuzi ili kutimiza azma ya uwekezaji bora
Tanzania.
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akizungumza wakati
wa uwekaji wa jiwe la msingi kuashiria ujenzi wa Kiwanda cha Keds
kilichopo Kibaha Mkoani Pwani.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Nchini, Clifford Tandari akizungumza
wakati wa uwekwaji wa jiwe la msingi katika Kiwanda cha Sabuni cha Keds.
Mkurugenzi wa Kiwanda hiko, Jack Feng akizungumza wakati wa uwekwaji wa jiwe la msingi katika Kiwanda cha Sabuni cha Keds.
Baadhi
ya viongozi mbalimbali na wanachi wakimsikiliza Waziri wa
Viwanda,Biashara na Uwekezaji,Mhe Charles Mwijage wakati wa uwekaji wa
jiwe la msingi kuashiria ujenzi wa Kiwanda cha Sabuni(Keds) kilichopo
Kibaha Mkoani Pwani.
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akiagana na
Mkurugenzi wa Kiwanda hiko,Jack Feng baada ya kuwasili katika Mkoani
Pwani.katikani Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji
Nchini,Clifford Tandari
Muonekano wa Mchoro kiwanda namna kitakavyo kuonekana baada ya kukamilika ujenzi wake.
No comments:
Post a Comment