Pages

January 17, 2017

MKUU WA MKOA WA ARUSHA MRISHO GAMBO AONGOZA KIKAO CHA WADAU KUMALIZA MGOGORO WA PORI TENGEFU LOLIONDO

Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo akiongoza kikao cha wadau wa kutafuta suluhu ya mgogoro wa matumizi ya ardhi katika Pori Tengefu la Loliondo uliofanyika Kijiji cha Wasso ukiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliyotoa katika ziara yake hivi karibuni mkoani humo.

Mbunge wa Jimbo la Ngorongoro ambaye ni Naibu Waziri wa Kilimo,Ufugaji na maendeleo ya Uvuvi,William Ole Nasha akizungumza katika mkutano huo ,kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo na Mwenyekiti wa CCM mkoa,Lekule Michael Laizer.

Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo akipokea nyalaka kutoka kwa  Mkazi wa Kijiji cha Wasso ,Tina Timan zilizowahi kutumika kutafuta suluhu ya mgogoro huo ambao eneo la Kilometa za mraba  1,500 lilitengwa kwaajili ya kuruhusu shughuli za uhifadhi ya wanyapori jambo linalopingwa na wenyeji.

Afisa Ardhi wa halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro,Kasema Samawa akifafanua namna wilaya hiyo ilivyopanga matumizi bora ya ardhi.

Diwani wa Viti Maalumu katika halmashari ya wilaya ya Ngorongoro,Kijoolu Kakeya akizungumza kwenye kikao kilichowakusanya wadau wote kujadili namna ya kupata suluhu ya mgogoro wa Pori Tengefu la Loliondo mkoa wa Arusha.

Mkazi wa Arash ,Rafael Long’oi akizungumzia namna anavyoufahamu mgogoro huo na namna ya kuumaliza kwa njia ya mazungumzo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...