Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni,
akipokea salamu za heshima baada ya kuwasili kituo cha Uhamiaji
Kasumulu, kinachosimamia masuala ya uingiaji na utokaji nchini kwa
wananchi wa Nchi za Tanzania na Malawi. Kulia ni Afisa Uhamiaji Mfawidhi
wa kituo hicho, Kamishna Msaidizi Taniel Magwaza. Naibu Waziri yupo
wilayani Kyela kwa ziara ya kikazi. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
(kushoto), akikagua hati ya kusafiria ya mwananchi kutoka nchi ya
Malawi, Miston Chikankheni aliyekuwa anaingia nchini katika Kituo cha
Uhamiaji Kasumulu, wilayani Kyela mkoa wa Mbeya. Naibu Waziri yupo
wilayani Kyela kwa ziara ya kikazi.
Mrakibu
Mwandamizi wa Idara ya Uhamiaji, Gragiza John akijibu maswali
aliyoulizwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhandisi Hamad Masauni (wapili kushoto) ,baada ya kutembelea moja ya
vipenyo vinavyopitisha wahamiaji haramu kutoka Malawi katika mpaka wa
Kasumulu. Naibu Waziri ameiagiza idara hiyo wakishirikiana na Jeshi la
Polisi kudhibiti njia hizo ili kuzuia uingiaji wa wahamiaji hao, wakati
wa ziara ya kikazi wilayani Kyela.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni,akumuuliza swali, Mrakibu Mwandamizi wa Idara ya Uhamiaji,
Gragiza John(kulia) wakati wa ziara yake ya kikazi ya ukaguzi wa
vipenyo vinavyotumiwa na wahamiaji haramu mpakani Kasumulu kuingia
nchini wakitokea Malawi. Naibu Waziri yupo wilayani Kyela kwa ziara ya
kikazi.
Mkuu
wa Idara ya Uhamiaji jijini Mbeya, Kamishna Msaidizi, Asumsio Achachaa,
akizungumza na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhandisi Hamad Masauni (kulia) baada ya kutembelea mpaka waKasumulu
unaotenganisha nchi za Tanzania na Malawi wilayani Kyela. Mlima
unaoonekana nyuma upo nchini Malawi. Naibu Waziri yupo wilayani Kyela kwa ziara ya kikazi.
Afisa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),
Lenny Mkola, akijibu swali lililoulizwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni linalohusiana na mapato kwenye mpaka wa Kasumulu unaotenganisha nchi
za Tanzania na Malawi. Naibu Waziri yupo wilayani Kyela kwa ziara ya kikazi.
IMEANDALIWA
NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI- WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
No comments:
Post a Comment