Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii Malinyi.
Halmashauri
ya Wilaya ya Malinyi ni moja ya Wilaya mpya hapa nchini zilizoundwa
kutokana na ukubwa wa mkoa wa Morogoro kwa lengo la kuzidi kuongeza
huduma za kiserikali kwa wananchi walio pembezoni hili kupunguza gharama
za wananchi kutembea umbali mrefu.
Malinyi
ambayo imezaliwa kutoka katika Wilaya Mama ya Halamashauri ya Wilaya ya
Ulanga ambayo ilionekana kubwa kuliko kawaida na kushindwa kukidhi
kuwahudumia wakazi wa malinyi kutokana na umbali wa kijiografia.
Mkurugenzi
wa halmashauri ya Wilaya ya Malinyi ,Marcelin Ndimbwa, akikagua ujenzi
wa madarasa ambayo yamejengwa kwa ajli ya watoto wa wafugaji Rumbanga.
Marceline
Ndimbwa ni Mkurugenzi wa kwanza katika halmashauri hiyo mpya kuteuliwa
na Rais wa awamu ya tano Daktari John Pombe Magufuli ili kuhakikisha
maendeleo ya wilaya hiyo yanafanana na sehemu nyingine.
Ndimbwa
amekuwa ni mkurugenzi wa halamashauri hiyo huku akikabiliana na
changamoto kubwa ya mgogoro wa ardhi baina ya wakulima na wafugaji na
changamoto ya miundombinu ya elimu katika jamii kubwa ya wafugaji.
Ndimbwa
anasema kuwa Rumbanga ni moja ya maeneo ambayo hayapo mbali na mji wa
Malinyi lakini yamekuwa na jamii kubwa ya wafugaji wa kabila la kisukuma
huku wakiwa na changamoto ya kutokuwa na shule ya msingi, Sekondari na
huduma za afya.
Ndimbwa
anasema kuwa mbali na changamoto zote hizo lakini ameamua kuanza na
changamoto kubwa ya kutokuwepo na shule ya msingi katika eneo hilo la
Rumbanga.
“kiukweli
hali sio nzuri katika eneo la Rumbanga kwani shule iliyopo ni ya nyasi
ambayo imejengwa na wanakijiji wenyewe na aina walimu wa kufundisha
zaidi vijana wawili ambao wamemaliza kidato cha nne na kuamua kujitolea
katika kuwafundisha wadogo zao ambao wapo kuanzia darasa la kwanza mpaka
la nne”amesema Ndimbwa.
Ndimbwa
anasema kuwa mara baada ya kuona mazingira hayo wakaona ni ulazima wa
kuamua kujenga shule hiyo kuwa ya kisasa kutokana changamoto ya umbali
kufata shule ambayo ipo kilometa 34 kutoka hapo Rumbanga na wanafunzi
hao kutakiwa kutembea kwenda na kurudi katika shule ya msingi Mwembeni
hali iliyochangia watoto wengi kuacha masomo na watoto wa kike kupata
ujauzito katikati ya masomo na kulazimika kuacha shule.
Anataja
kuwa katika hatua za awali zilizochukuliwa na halmashauri yake katika
kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi na sera ya Rais Magufuli ya
kupata elimu bure na sio bure tu bali iliyobora kwa wanafunzi, Serikali
ya Wilaya imeamua kubuni arambee kutoka kwa jamii ya wafugaji na kutenga
fedha kadhaa kwa ajili ya kujenga majengo ya kisasa ya shule ya msingi
Rumbanga ambayo imeanza kutokana na jitahada za watu wa jamii hiyo ya
wafugaji.
“hatua
ya kwanza niliyochukua ni kuchukua fedha za zilizotengwa kwa ajili ya
kwenda Simiyu kuzima mwenge kiasi cha shilingi milioni 4 zipelekwe
Rumbanga kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo hivyo kuongeza hali ya mwamko
kwa wakazi wa kijiji hicho chenye jamii ya wafugaji” anasema Ndimbwa.
Ndimbwa
anasema wanafunzi hawa pindi shule zitakapofungua awatasoma tena katika
mabanda ya nyumba za nyansi kama ilivyokuwa awali hivyo watakingi
katika madarasa ya kisasa kama ilivyo kwa watoto wengine wa Tanzania.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Malinyi, Nasoro
Liguguda amesema kuwa uamuzi huo wa mkurugenzi wa mtendaji wa
halmashauri umekuja wakati muafaka kwani jamii kubwa ya watoto wa
wafugaji walikuwa wakiteseka kwa kupata elimu bora kutokana na wao
kupendelea kuishi pembezoni na kuanzisha miji mipya.
Anasema
wafugaji hao ambao kwa sasa wameamua kuishi malinyi hapo ni vyema nao
wakapata stahiki zao za huduma za jamii kama ilivyo kwa jamii ya
wakulima hili kupunguza migogoro.
Nae
katibu wa kamati ya ujenzi wa shule hiyo, Joseph Paschal wanashukuru
halmashauri kwa kuweza kuwapatia fedha za kujenga shule hiyo ambayo ni
tumaini jipya kwa wakazi wa Rumbanga .
Anataja
kuwa wakazi wa kijiji hicho walikuwa wakikumbwa na chngamoto nyingi
wakati wa masika pindi wanapohitaji kwenda shule kutokana na kushindwa
kuvuka mto Rumbanga ambao mara zote uwa unajaa maji hivyo kukusa masomo
kwa kipindi chote.
Kwa
upande wake mkurugenzi Ndimbwa amesema kuwa serikali imekwisha ridhia
kuiweka shule hiyo katika mpango ujao wa bajeti lakini kwa sasa shule
hii itakuwa kama shule dada ya shule ya miembeni mpaka hapo itakapo pata
usajili kamili.
Hivyo
ametaja wazi kuwa shule hiyo ambayo itakuwa na miundombinu ya kisasa na
ujenzi wa choo bora ambacho kitajengwa sambamba na Zahanati ya Lumbanga
ambayo itajenga jirani na eneo hilo la shule.
Mkurugenzi
wa halmashauri ya Wilaya ya Malinyi ,Marcelin Ndimbwa, akikagua
madarasa ambayo yamejengwa kwa ajli ya watoto wa wafugaji Rumbanga.
Mkurugenzi wa malinyi,Marcelin Ndimbwa, akionyesha choo kilichokuwa kikitumiwa na wanafunzi hao.
sehemu ya ubao wa kufundishia wa shule hiyo ya manyasi.
mkurugenzi wa malinyiMarcelin Ndimbwa akitoka darasani katika shule ya msingi Rumbanga.
No comments:
Post a Comment