Wapatanishi
katika Jamhuri wa Kidemokrasia ya Congo, wameandaa mwafaka wa
kuhakikisha kuwa madaraka yanapokezwa kwa njia ya amani.
Mashauriano
yaliyoandaliwa na Kanisa Katoliki, yanafuatia kukataa kwa Rais Joseph
Kabila, kuondoka madarakani baada ya utawala wake wa mihula miwili
kukamilika.
Chini ya mapatano hayo Rais Kabila ataendelea kuwa Rais hadi wakati wa uchaguzi ifikapo mwisho wa mwaka ujao.
Waziri Mkuu
mpya atachaguliwa kutoka kwa upande wa upinzani na mpango huo
utasimamiwa na mkongwe wa upinzani, Etienne Tshisekedi.
Mwandishi wa
habari wa BBC, alisema kuwa ingawa kuna ripoti kuwa pande kinzani
zimekubaliana kwa maswala fulani, haiwezekani sahihi za mkataba huo
kutiwa sahihi kabla Krismasi.
Kukataa kwa
Bwana Kabila kuondoka madarakani na kuahirishwa kwa uchaguzi
kumesababisha maandamano makali katika barabara kuu za miji nchini
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
No comments:
Post a Comment