Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
HISTORIA
ya watumwa na kuanza kwa dini ya kikristo visiwani Zanzibar yawa
kivutio kikubwa sana kwa watalii kutoka nchi mbalimbali kwa kufika
katika Kanisa la The Cathedral Church of Christ lilijengwa na Bishop
Edward Sterre kufahamu undani wakuja kwa dini hiyo kwneye visiwa hivyo.
Kanisa
hilo limejengwa lilipokuwa Soko la watumwa lilijojengwa mwisho wa karne
ya 19 pakitumika kama eneo la kuhifadhi watumwa wanaotolewa maeneo
mbalimbali na Zanzibar ikiwa ndio kitivo cha biashara hiyo na Bishop
Edward Sterre akaamua kuwanunua watumwa hao kwa
lengo la kukomesha biashara ya utumwa na wakati wa ujenzi wa jengo la
kanisa watumwa walitumika kujenga na ikiwa ni kama kuwakomboa na kisha
baadae kuwabatiza na kuwa wakristo.
Kwa
sasa kanisa hilo linaweza kupokea wageni kutoka mataifa mbalimbali
wanaoenda kufahamu historia ya watumwa na kuanza kwa dini ya kikristo
pia kuna huweza kufika 1000 kwa siku kulingana na kipindi kilichopo.
Katika
chumba kimoja cha watumwa walikaa takribani 75 yaani watoto 25 na
wakubwa 50 na waliweza kukaa humo kwa kipindi kisichopungua siku mbili
hadi tatu na wengine walikufa kutokana na kukosa hewa pamoja na
kutokupewa chakula, mbali na hilo pia walifariki kwa magonjwa ya mlipuko
kwani walikuwa wakilala juu ya kibaraza lakini kwa chini wakawa
wanatumia kama sehemu ya haja ndogo na kubwa wakisubiri maji yajae
baharini ili yaingie na kusafisha.
Picha za maeneo ya kanisa hilo liliopo eneo la Darajani Mkunazini Visiwani Zanzibar.
The
Cathedral Church ambapo kabla ya kuwa kanisa lilitumika kama soko la
watumwa visiwani humo wakiletwa kutoka sehemu tofauti kwa ajili ya
biashara hiyo.
Muonekano wa nje wa The Cathedral Church of Christ lilijengwa na Bishop Edward Sterre lililojengwa karne ya ya 19 kwa lengo la kukomesha biashara ya utumwa.
Kanisa la Thed Cathedral Church of Christ katika muonekano wake wa ndani.
Wageni
mbalimbali wakiwa wametembelea kanisa hilo na kufahamu historia ya
watumwa iliyokuwa imeshamiri visiwani Zanzibar na kuanza kwa dini ya
kikristo.
Kinandsa cha kwanza kutumika katika kanisa hilo na kinapatikana katika nchi kadhaa barani Afrika ikiwamo Visiwa vya Zanzibar.
Kinanda
kingine kilichokuwa kinatumika kanisa hapo pamoja na kuharibika bado
kinaendelea kutumia kwa ibada na kinafanya kazi kama kawaida.
Kinu
kilichojengwa ndani ya Kanisa hilo ambapo kilikuwa kinatumika kwa ajili
ya kubatiza watumwa na baadae kuanza kutumika kwa ajili ya watoto.
Moja ya chumba walichokuwa wanakaa watumwa wanawake na watoto 75 na walikaaq humo kwa siku mbili hadi tatu.
Njia
inayoelekea kwenye vymba vilivyokuwa vinatumika kukaa kwa watumwa
ambapo Bishop Edward Sterre aliamuru sehemu hii ndiyo ijengwe kanisa.
Picha ya Bishop Bishop Edward Sterre ikiwa ndani ya kanisa hilo.
Chini ni kaburi lake likiwa nyuma ya madhabahu ambapo alizikwa.
No comments:
Post a Comment