Nteghenjwa Hosseah, Arusha
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ameitaka Wizara ya Mifugo, Chakula na
Ushirika kuacha kutoa vibali vya kusafirisha mahindi nje ya nchi kwa
wafanyabiashara wa hapa nchini kwani Serikali Mkoani Arusha ilishapiga
marufuku usafirishwaji wa mahindi hayo nje ili kulinda viwanda vya hapa
nchini.
Mhe.
Gambo alisema hayo jana baada ya kutembelea maghala matatu ya Wakala wa
Taifa wa Hifadhi ya Chakula{NFRA} Kanda ya Arusha kujionea hali halisi
ya uhifadhi wa mahindi katika maghala hayo na kuskiliza changamoto zake
na kukuta tani 6,620 za mahindi zilizoko kwa sasa.
Alisema
serikali Mkoani Arusha ilishapiga marufuku uuzwaji wa mahindi nje ya
nchi lakini kuna baadhi ya wafanyabiashara wamekamatwa na vyombo vya
ulizni na usalama wakiwa na vibali kutoka Wizarani vinavyowaruhusu
kupeleka mahindi nchi jirani ya Kenya hali inayowafanya watendaji wa
serikali kushindwa kufanya kazi kutokana na mkanganyiko huo.
Mkuu
huyo alisema uamuzi wa kupiga marufuku uuzwaji mahindi nje ulitolewa na
serikali kuu na Mkoa ulisimamia hilo kwa lengo la kuvilinda viwanda vya
hapa nchini kwa uzalishaji wa bidhaa hivyo na kunufaika na unga na pumba
za mahindi tofauti na ilivyo sasa.
Alisema
kutokana na mkanganyiko huo aliwaomba watendaji wa Wizara kuacha kutoa
vibali kwa wafanyabiashara kuuza mahindi nje ili kuwasaidia wenye
viwanda vya nafaka kuuza unga na pumba nje wenye kiwango ili nao waweze
kupata faida na nchi iweze kupata faida zaidi.
Mhe.
Gambo alisema mbali ya hilo pia serikali Mkoani Arusha imefanikiwa
kuziba njia zote za panya zilizokuwa zikitumika na wafanyabiashara
kutorosha mahindi kwenda nchi jirani ya Kenya na kusema kuwa hilo nalo
linapaswa kuungwa mkono na Wizara ili amri hiyo iweze kutekelezeka.
‘’Vibali
vya Wizara kwa wafanyabiashara kuuza mahindi nje vinatuchanganya sana
na vinapingana na amri yetu na nchi kwa ujumla na kutokana na hali hiyo
tunaiomba wizara iache kufanya hivyo kwa maslahi ya nchi na
wafanyabishara wa ndani ili waweze kuuza unga badala ya mahindi kwani
watanufaika zaidi’’alisema Gambo
Naye
Meneja wa NFRA Kanda ya Arusha, Abdillah Nyangasa alikitoa taarifa kwa
Mkuu wa Mkoa, alisema kuwa zoezi la ununuzi lililoanza agosti 25 mwaka
jana na kumalizika novemba 30 mwaka huo huo malengo yalikuwa kununuwa
mahindi tani 15,000 lakini walifanikiwa kununuwa mahindi tani 5,111 tu
na hiyo ni kutokana na ufinyu wa bajeti.
Nyangasa
alisema changamoto iliyowakabili katika kipindi cha ununuzi kipindi
hicho ilikuwa uzalishaji mdogo wa nafaka hususani mahindi ambo haukwenda
sambasamba na mahitaji au matumizi ya kukidhi nchi na hali hiyo
ilichangia sana bei ya mahindi au unga kupanda kwa kasi kubwa kwenye
soko lake karibu nchi zima.
Alisema
changamoto nyingine ni udhibiti mdogo wa soko la mahindi kwenye maeneo
ya mipakani kwani kumekuwa na njia nyingi zizizo rasmi maarufu kwa njia
ya panya kwa mikoa ya Arusha na Kilimanjaro na mahindi mengi yamevuka
kwenda nchini Kenya kitu ambacho yangesaidia sana uhaba mkubwa wa
chakula ulioko sasa endapo yangedhibitiwa.
Meneja
huyo alisema kutokana na ununuzi mdogo wa mahindi Kanda ya Arusha NFRA
makao makuu inaanga lia uwezekano wa kuongeza akiba hiyo kwa kuhamisha
sehemu ya akiba yake kutoka katika kanda zake za Nyanda za Juu Kusini
ambazo ununuzi wake ulikuwa wa kuridhika kidogo.
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo (Pili kushoto) akiwasili
katika Ofisi za Wakala wa Taifa wa Uhifadhi wa Chakula Kanda ya
Kaskazini zilizoko Mkoani Arusha kuangalia na kukagua hali ya uhifadhi
wa Chakula.
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo(kwanza kushoto) pamoja na Meneja wa
NFRA Kanda ya Kaskazini Ndg.Abdillah Nyangasa wakitembelea maghala ya
kuhifadhia Chakula wakati wa ziara yake katika Ofisi hizo.
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo(kwanza kulia) akikagua taarifa za
mazao yaliyohifadhiwa katika Magahala ya NFRA wakati wa ziara yake ya
kukagua hali ya Uhifadhi wa Chakula.
Kutoka
kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Ndg. Richard Kwitega
akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo na Meneja wa NFRA
Ndg. Abdillah Nyangasa wakati wa kikao na wafanyakazi wa NFRA Kanda ya
Kasikazini.
No comments:
Post a Comment