Pages

January 6, 2017

DC AINGILIA KATI MGOGORO WA WAFUGAJI NA MWEKEZAJI WA SHAMBA LA MKONGE MARUNGU MKOANI TANGA

 Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akizungumza wakati wa mkutano wa wananchi wa Kijiji cha Marungu ambao ni sehemu ya waathirka na mgogoro huo sambamba na muwekezaji wa shamba hilo na kusema kuwa makubaliano yaliyofikiwa baina ya serikali na wafugaji hao lazima yatekelezwe kwa wakati ili kuepusha vurugu za uvunjifu wa amani uliokuwa ukijitokeza mara kwa mara.
 Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga(DAS),Faidha Salim akizungumza katika mkutano huo
 Diwani wa Kata ya Marungu (CCM) Mohamed Mambea akizungumza wakati wa mkutano huo
 Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa katikati akiandika baadhi ya maswali ya wananchi ambao walikuwa wakiuliza kwenye mkutano huo.
 Wananchi wakifuatilia mkutano wa hadhara wa Mkuu huyo wa wilaya.




MKUU wa Wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa ameingilia kati mgogoro wa wafugaji na mwekezaji wa shamba la mkonge la Marungu Mkoani Tanga na kutoa miezi mitatu kwa wafugaji hao kuhakikisha wanaondoka katika shamba hilo kabla ya serikali haijatumia nguvu ya kuwahamisha.


Akizungumza katika kikao cha wananchi wa Kijiji cha Marungu ambao ni sehemu ya waathirka na mgogoro huo sambamba na muwekezaji wa shamba hilo na kusema kuwa makubaliano yaliyofikiwa baina ya serikali na wafugaji hao lazima yatekelezwe kwa wakati ili kuepusha vurugu za uvunjifu wa amani uliokuwa ukijitokeza mara kwa mara.


Maamuzi hayo yamekuja ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo lililotolewa siku chache zilizopita na Mh;WAziri MKuu la kuwataka Wakuu wote wa Wilaya nchi nzima kuhakikisha wanamaliza migogoro ya ardhi iliyondani ya uwezo wao ili kutoa fursa kwa wananchi kuendelea na shughuli zao.


Mwilapwa alisema kumekuwepo na madhara mengi yanayojiketokeza kutokana na kuwepo kwa migogoro ya wakulima na wafugaji hadi kufikia kutokea mapigano yanayohatarisha amani iliyopo baina ya makundi hayo mawili jambo ambalo serikali imejidhatiti kumaliza migogoro hiyo kwa makubaliano ya mazungumzo.


“Kumekuwepo na mapigano ya mara kwa mara baina ya wakulima,mwekezaji na wafugaji jambo linalovunja amani na hata kuhatarisha maisha ya watu nisema ikiwa makubaliano haya hayatatekelezwa basi Serikali itaingilia kati na itawahamisha wafugaji hao kwa nguvu”Alisema Mwilapa.


Kwa upande wa Diwani wa kata ya Marungu Mohamed Mwambea alisema kuwepo kwa wafugaji hao katika shamba hilo ndani Kijiji hicho kumeleta madhara makubwa kutokana na kutokea mapigano  kwa pande hizo mbili na kutokea uharibifu wa mazao ya wananchi wanaojishughulisha na kilimo Kijijini hapo.


Mwambea alisema imekuwa kawaida kwa wafugaji kushinda katika kesi zao dhidi ya wakulima jambo linaloshangaza wanapata wapi haki ya kuweza kushinda kila aina ya kesi zinazojitokeza baina ya wakulima na wafugaji.


“Ifike wakati kwa Serikali iwe inatenda haki kwa wakulima dhidi ya wafugaji ili kujenga usawa kwa jamii hizo mbili ambazo zinaingia katika migogoro inayohatarisha maisha yao na hata jamii inayotuzunguka”Aalisema Mwambea.


Nae Meneja wa shamba la mkonge la Marungu Casmir Joackim alisema wameshindwa kuendelea na uzalishaji katika shamba hilo kwa zaidi ya miaka miwili kutokana kuingiliwa na wafugaji hao waliohamishia shughuli zao za kifugaji na makazi katika shamba hilo.


Joackim alisema dhamira ya muwekezaji wa shamba hilo ni kutekeleza agizo la Serikali ya awamu ya tano ya kuwataka wawekezaji wote nchini wayaendeleze mashamba yao kiuzalishaji na hata kutoa ajira kwa wananchi ili kukwepa mkono wa Serikali unaoweza kufuta hati ya umili wa shamba hilo na kurudishwa serikalini kwa ajili ya kugawiwa upya wananchi.


“Ikiwa ndani ya shamba letu wapo wafugaji wanaendelea na shughuli zao za ufugaji pamoja na maisha kwa ujumla tangu mwaka 2014 ni namna gani tunaweza kundeleza shughuli zetu,huoni mkono wa Serikali unaweza kutukumba lazima tutendewe haki kwa hawa watu ambao ni wavamizi”Alisema Joackim.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...