Amisi Tambwe akipambana na beki wa Azam Yahaya Mohamed wakati wa mchezo wa hatua ya makundi wa kombe la Mapinduzi uliomalizika kwa Azam kutoka na ushindi wa goli 4-0.
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Timu
ya Azam Fc imefanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali kwa kuipa kipigo
cha mbwa mwizi cha bao 4-0 timu ya Yanga huku wakikalia usukani mwa
kundi B katika kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar usiku huu.
Mpira ulianza kwa kasi ikionekana Azam FC wamepania kupata bao la mapema Dakika ya kwanza ya mchezo na katika dakika
ya 2 Azam wanapata bao kupitia kwa mfungaji wao John Bocco baada ya
kutokuwa na maelewano baina ya mabeki wa Yanga kwenye kuuokoa mpira
uliookolewa na golikipa wa Yanga, Deogratius Munish "Dida".
Katika
dakika ya 9 Yanga wanafanya shambulizi langoni mwa Azam lakini Saimon
Msuva anashindwa kumalizia kazi nzuri iliyofanywa na mrundi Amisi
Tambwe.
Baada ya kuonekana kutokuwa na maelewano katika safu ya ushambuliaji Kocha George Lwandamina anafanya mabadiliko kwa kumtoa Juma Mahadhi na nafasi yake inachukuliwa na Emmanuel Martin katika dakika ya 36. Mpaka Mapumziko Azam 1 Yanga 0.
Kipindi
cha pili kinaanza kwa kila mmoja kumsoma mwenzake lakini katika dakika
ya 54, Yahaya Mohamed anaipatia Azam goli la pili baada ya kuunganisha
krosi safi Abubakar Salum " Sure Boy".
Wakiwa
bado hawaamini Dk 81, Joseph Mahundi anaiandikia Azam goli la tatu
baada ya kuachia shuti kali nje ya 18 na kuacha mashabiki wa Yanga
wakiduwaa wakiwa hawaamini wanachokiona.
Dk
84, Atta aliyeingia kipindi cha pili anaifungia timu yake bao safi
akiunganisha pasi ya Afful baada ya Mwashiuya kuukosa mpira, na mpaka
mpira unamalizika Azam wanatoka kifua mbele wakiwa na alama 7
wakifuatiwa na Yanga wenye alama 6.
Timu hizi zinasubiri washindi wa mechi za kesho kwenye kundi A ili kupambana nazo kwenye hatua ya nusu fainali.
Kikosi cha Yanga kilichopambana usiku huu.
Kikosi cha Azam kilichopambana usiku huu.
Wachezaji wakiwa wanafanya mazoezi kabla ya mechi.
Timu zikiingia uwanjani wakati wa mchezo wa hatua ya makundi kati ya Yanga na Azam
Saimon
Msuva akimtoka beki wa Azam wakati wa mchezo wa hatua ya makundi wa
kombe la Mpoinduzi uliomalizika kwa Azam kutoka na ushindi wa goli 4-0.
Juma
Mahadhi akipambana katikati ya mabeki wa Azam wakati wa mchezo wa hatua
ya makundi wa kombe la Mpoinduzi uliomalizika kwa Azam kutoka na
ushindi wa goli 4-0.
Frank
Domayo (kushoto) akipambana na kiungo wa Yanga Haruna Niyonzima wakati
wa mchezo wa Azam na Yanga uliomalizika kwa Azam kushinda 4-0.
Wachezaji wa Azam wakishangilian moja ya goli lilofungwa katika mchezo huo leo usiku.
Kiungo
wa Yanga Justine Zulu akiwa amebebwa na golikipa wa Yanga Ally Mustafa
'Batez' baada ya kuumia wakati wa mchezo huo na kutolewa nje.
No comments:
Post a Comment