Vijana
wanaotoka katika halmashauri za wilaya ya Kahama Mji, Ushetu, Msalala
na Manispaa ya Shinyanga wamekutana katika bonanza la michezo
lililoandaliwa na Shirika la Kitanzania lisilo la kiserikali la Ariel
Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative (AGPAHI) linalojihusisha na
mapambano dhidi ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI.
Bonanza hilo la michezo limejumuisha vijana 150 wenye umri kati ya miaka
14-19 wanaotoka katika klabu za vijana zilizoundwa na zinasimamiwa na
shirika la AGPAHI kwa kushirikiana na halmashauri za wilaya husika.
Akifungua bonanza hilo katika uwanja wa taifa mjini Kahama leo Jumamosi
Desemba 17,2016,mgeni rasmi Dr. Anthony Kasomelo kutoka hospitali ya mji
wa Kahama,alisema bonanza hilo ni kwa ajili ya vijana
kufurahi,kufahamiana,kupata marafiki wapya,kuonyesha vipaji na
kujifunza.
"Vijana hawa wanatoka kwenye vikundi 12 vilivyopo katika halmashauri nne
za mkoa wa shinyanga,ambazo ni Msalala,Kahama mji,Ushetu na manispaa ya
Shinyanga", alisema Kasomelo.
Dr.
Kasomelo alitumia fursa hiyo kulipongeza shirika la AGPAHI kwa
kuendelea kuwa karibu na vijana huku akiwaasa vijana hao kuendelea kuwa
wafuasi wazuri wa huduma za afya ili kuboresha afya zao ili waweze
kutimiza ndoto zao.
Aidha alitoa wito kwa viongozi wa halmashauri za wilaya kuendelea kutoa
ushirikiano kwa shirika la AGPAHI hasa katika kutekeleza majukumu ya
kuwasaidia wananchi katika huduma za afya hususani kwa watu wanaopata
tiba na matunzo ili huduma zipatikane katika ubora na ziwe rafiki kwa
wananchi.
Awali akizungumza katika bonanza hilo, Afisa mradi wa watoto kutoka
Shirika la AGPAHI mkoa wa Shinyanga, Jane Kashumba alisema wafadhili wa
bonanza hilo ni shirika la Uingereza linalofadhili huduma za kuboresha
maisha ya watoto (Children's Investment Fund Foundation -CIFF).
Kashumba alibainisha kuwa shirika la AGPAHI limeanzisha klabu 12 za
vijana zenye wastani wa vijana 20 - 70 walio katika rika balehe.
"Lengo
la vikundi hivi ni kuwakutanisha vijana kila mwezi ili waweze kujifunza
pamoja masuala mbalimbali ikiwemo masuala ya msukumo rika kwa
vijana,kushirikiana katika kutatua changamoto zao na njia za kujikinga
na maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi vijana hao wameendelea
kunufaika na elimu hiyo",alieleza Kashumba.
Miongoni
mwa michezo iliyochezwa na vijana hao ni pamoja mpira wa miguu,kuvuta
Kamba,mbio za magunia,kukimbiza kuku ,kuimba nyimbo na kucheza muziki
ambapo washindi waliibuka na zawadi mbalimbali.
Bonanza
hilo limehudhuriwa na wadhibiti wa Ukimwi kutoka halmashauri za
wilaya,wasimamizi wa klabu za vijana,wafanyakazi wa shirika la AGPAHI na
wadau mbalimbali wa michezo na mambo ya afya.
Angalia matukio katika picha yaliyojiri uwanjani hapa chini
Afisa
mradi wa watoto kutoka Shirika la AGPAHI mkoa wa Shinyanga, Jane
Kashumba akizungumza wakati Bonanza la michezo katika uwanja wa taifa wa
mjini Kahama
Mgeni
rasmi Dr. Anthony Kasomelo kutoka hospitali ya mji wa Kahama akifungua
bonanza hilo la vijana lililokutanisha vijana 150 ambapo mbali na
kulipongeza shirika la AGPAHI alitumia fursa hiyo kuwaasa vijana hao
kupenda shule
Mgeni
rasmi Dr. Anthony Kasomelo akizungumza wakati wa kufungua bonanza la
michezo.Kushoto ni Mhudumu wa jamii pia Afisa tabibu kutoka kituo cha
afya cha Kolandoto katika manispaa ya Shinyanga Maryciana Bruno
,aliyeinama kulia ni Mganga mfawidhi zahanati ya Segese Denis Ngatale
Mgeni rasmi Dr. Anthony Kasomelo akiteta jambo na Jane Kashumba
Timu
ya mpira wa miguu kutoka halmashauri ya manispaa ya Shinyanga
wakijiandaa kuanza mchezo baina yao na timu kutoka halmashauri ya wilaya
ya Ushetu,Msalala na Kahama Mji.
Wachezaji wa timu ya mpira wa miguu kutoka manispaa ya Shinyanga wakiwa na walezi wao na maafisa kutoka AGPAHI
Wachezaji wa timu ya mpira wa miguu kutoka halmashauri ya wilaya ya Ushetu,Msalala na Kahama Mji wakipiga picha kabla ya mchezo
Wachezaji wa timu ya halmashauri ya wilaya ya Kahama Mji,Ushetu na Msalala wakiwa na walezi wao na maafisa kutoka AGPAHI
Dawati la ufundi timu ya Kahama Mji,Ushetu na Msalala.
Mchezo kati ya Kahama Mji,Ushetu na Msalala ukiendelea
Mchezo
unaendelea ambapo hadi kipenga cha mwisho kinapulizwa Kahama mji
walikuwa wanaongoza kwa kuibamiza timu ya manispaa ya Shinyanga bao 4-1
Mbio
za magunia ukiendelea kati ya vijana wa kike kutoka manispaa ya
Shinyanga(waliovaa nguo za bluu) na wasichana kutoka Kahama Mji,Ushetu
na Msalala zikiendelea
Mbio
za magunia zikiendelea ambapo hadi mwisho wa mchezo mshindi wa kwanza
alikuwa Esther Peter kutoka Ushetu (aliyevaa nguo nyeupe),wa pili
Elizabeth Busheye kutoka manispaa ya Shinyanga(wa kwanza kulia)
Mbio
za magunia upande wa vijana wa kiume kutoka manispaa ya Shinyanga
(waliovaa nguo za bluu) na wasichana kutoka Kahama Mji,Ushetu na Msalala
zikachukua nafasi
Mchezo unaendelea,ambapo hadi mwisho wa mchezo mshindi wa kwanza alikuwa Ali Seleman,wa pili Isack Kiwila
Mchezo wa kufukuza kuku upande wa vijana wa kike ukiendelea
Vijana wakiendelea kukimbiza kuku
Helena
Daudi kutoka manispaa ya Shinyanga akiwa amebeba kuku baada ya
kufanikiwa kumkamata na kisha kuondoka naye kama zawadi ya ushindi
Vijana wa kiume nao walifukuza kuku
Kijana Peter Kulwa naye akaondoka na kuku baada ya kufanikiwa kumkamata
Mchezo
wa kuvuta kamba nao ulikuwepo,picha ni kushoto ni vijana wa kike kutoka
Kahama mji,Ushetu na Msalala wakijiandaa kushindana kuvuta kamba na
vijana wa kike kutoka manispaa ya Shinyanga(kulia).Waliopo katikati ni
Dr. Anthony Kasomelo kutoka hospitali ya mji wa Kahama na Afisa mradi wa
watoto kutoka Shirika la AGPAHI mkoa wa Shinyanga, Jane Kashumba
wakitoa maelekezo kwa vijana hao kabla ya mchezo huo wa kuvuta kamba
Vijana kutoka manispaa ya Shinyanga wakijiandaa kuvuta kamba
Katika mchezo huo wa kuvuta kamba vijana kutokaUshetu,Msalala na Kahama Mji waliibuka washindi
Vijana
wa kiume kutoka Kahama Mji,Ushetu na Msalala wakijiandaa kushindana
kuvuta kamba dhidi ya vijana kutoka manispaa ya Shinyanga
Vijana kutoka manispaa ya Shinyanga wakikazana kuvuta kamba ingawa hata hivyo walishindwa katika mchezo huo
Vijana kutoka manispaa ya Shinyanga wakiimba shairi
Walezi wa vijana na vijana wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea uwanjani
Vijana kutoka Kahama mji wakiimba
Kulia
ni Dr. Selemani Wambili kutoka Zahanati ya Kagongwa wilayani Kahama na
mlezi wa vijana kituo cha Segese katika halmashauri ya Msalala
wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea
Vijana wakiwa eneo la tukio
Vijana kutoka manispaa ya Shinyanga wakicheza muziki
Vijana wakionesha kipaji cha kucheza
Kijana akiimba wimbo
Vijana wakishindana kucheza muziki
Wajumbe
wa kamati ya kutoa zawadi kwa washindi katika michezo iliyofanyika
uwanjani wakijadili jambo kabla ya kuanza kugawa zawadi kwa
washindi.Aliyekaa kushoto ni Dr. Selemani Wambili kutoka Zahanati ya
Kagongwa,kulia kwake ni mhudumu wa jamii kutoka kituo cha Kolandoto
Maryciana Bruno.Waliosimama wa kwanza ni kushoto ni mlezi wa watoto
kituo cha Kambarage Glory Assey akifuatiwa na mlezi wa watoto kituo cha
hospitali ya Kahama mji Flora Selutongwe.Kulia ni mgeni rasmi Dr.
Anthony Kasomela akijiaandaa kupokea majina ya washindi ili awape zawadi
Mgeni
rasmi Dr. Anthony Kasomelo akitoa zawadi ya kombe kwa Timu ya Kahama
mji,Ushetu na Msalala walioibuka washindi baada ya kuifunga timu ya
manispaa ya Shinyanga bao 4-1
Vijana wakifurahia baada ya kupewa zawadi ya kombe
Vijana waliofunga magoli manne na kuipa ushindi timu ya Kahama mji,Ushetu na Msalala wakipokea zawadi ya saa kila mmoja
Vijana kutoka manispaa ya Shinyanga wakipokea zawadi kombe kwa kuibuka wachezaji bora wa muziki
Mgeni
rasmi Dr. Anthony Kasomelo akimkabidhi zawadi ya saa Esther Peter kutoka
Ushetu aliyekuwa mshindi wa kwanza katika shindano la mbio za magunia
Mshindi wa pili mbio za magunia upande wa vijana wa kike Elizabeth Busheye kutoka manispaa ya Shinyanga akipokea zawadi ya saa
Mshindi wa kwanza mbio za magunia upande wa vijana wa kiume Ali Seleman kutoka manispaa ya Shinyanga akipokea zawadi ya saa
Mshindi
wa pili mbio za magunia Isack Kiwila kutoka manispaa ya Shinyanga
akishikana mkono na mgeni rasmi kabla ya kupokea zawadi ya saa
Kijana aliyeonesha kipaji cha kucheza muziki akipokea zawadi ya begi
Mlezi
wa vijana katika kituo cha hospitali ya mkoa wa Shinyanga Elizabeth
Lubasha akijiandaa kupokea vifaa vya shule ikiwepo soksi na kalamu kwa
ajili ya vijana anaowalea
Mlezi wa vijana katika kituo cha Segese Kanzaga Fabian akipokea vifaa vya shule kwa ajili ya vijana wake
Mlezi
wa watoto kituo cha hospitali ya Kahama mji Flora Selutongwe akiwa
amebeba zawadi ya soksi na kalamu kwa ajili ya vijana anaowalea. Picha
zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
No comments:
Post a Comment