Benki kuu
ya Tanzania inapenda kuwafahamisha wananchi wote kuwa,habari inayoenea
katika mitandao mbalimbali ya kijamii kwamba noti ya shilingi mia tano
haitatumika tena kuanzia Desemba 31,2016; sio taarifa ya kweli na ni
uvumi unaopaswa kupuuzwa. Ukweli ni kwamba noti ya shilingi 500
itaendelea kuwepo katika mzunguko sambamba na ile sarafu ya shilingi 500
hadi pale noti hiyo itakapotoweka mikononi mwa wananchi. Tafadhali
mpuuze taarifa hizo sio za ukweli. Marcian Kobello. Mkurugenzi wa Huduma
za kibenki- BoT .
No comments:
Post a Comment