Pages

December 23, 2016

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO AKABIDHI MADAWATI NA VIFAA VYA USAFI SHULE YA MSINGI CHEMKA

Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC)Dk Richard Massika akizungumza katika hafla ya kukabidhi Madawati na kuzindua Vituo vya kunawia mikono vya wanafunzi hao kwa ufadhili wa Chuo cha  ATC cha jijini Arusha katika Shule ya Msingi Chemka,Kata ya Rundugai wilaya ya Hai mkoa wa Kilimanjaro.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Meck Sadick(kulia) na Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa wakizungumza jambo na baadhi ya wafanyakazi wa Chuo cha Ufundi Arusha.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Meck Sadick( wa pili kulia) akisalimiana na Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Chemka katika Kata ya Rundugai wilaya ya Hai,Fadhil Mwidini wakati wa ziara yake kukabidhi Madawati na kuzindua vituo vya kunawa miko vya wanafunzi hao,kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa.


Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa(kulia)akizungumzia umuhimu wa Vituo vya kunawa mikono kwa wanafunzi wa Shule hiyo,kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Meck Sadick

Mmoja wa wanafunzi akinawa mikono yake iwe safi ili kuepuka maradhi yanayosababishwa na mikono kutokuwa safi.

Wanafunzi  wakiwa wamejumuika na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Said Meck Sadick,Mkuu wa Chuo cha ATC,Dk Richard Massika na Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa kukalia madawati yaliyokabidhiwa kwa Shule hiyo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...