Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani (Wa
tatu kulia) akijadiliana jambo na Mkandarasi wa kampuni ya Rv associates
India& AES Tanzania anayejenga Daraja la Kilombero. Daraja hilo
lipo katika barabara kuu ya Ifakara –Mahenge Mkoani Morogoro.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani
amemuagiza Mkandarasi wa kampuni ya Rv associates India & AES
Tanzania anayejenga daraja la Kilombero lenye urefu wa mita 384
kukamilisha ujenzi huo mapema ifikapo januari mwakani ili daraja hilo
lianze kutumiwa na wananchi wa Mkoa wa Morogoro.
Mhandisi
Ngonyani ametoa agizo mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa
daraja hilo lenye urefu wa mita 384 linalounganisha barabara kuu ya
Ifakara –Mahenge mkoni Morogoro.
“Wananchi
wa Ifakara wanahamu ya kuona daraja hili linakamilika na kuanza
kutumika mapema, hivyo ongezeni kasi ya ujenzi wa daraja hili ili
likamilike haraka na kwa ubora uliokusudiwa ili liweze kudumu na
kutumika kwa muda mrefu”. amesisitiza Mhandisi Ngonyani.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani (Wa
kwanza kushoto) akipata maelezo Ujenzi wa Daraja la Kilombero kutoka kwa
Mkandarasi wa kampuni ya Rv associates India& AES Tanzania. Daraja
hilo lipo katika barabara kuu ya Ifakara –Mahenge Mkoani Morogoro.
Ameongeza
kuwa kukamilka kwa daraja hilo kutawafanya wananchi kuachana na usafiri
wa kutumia kivuko cha Mv. Kilombero ambacho wakati wa mvua kubwa
hushindwa kutoa huduma za usafiri kwa wananchi hao na hivyo kukwamisha
shughuli zao za kimaendeleo.
Katika
hatua nyingine Mhandisi Ngonyani amekagua barabara ya kuu ya kitaifa
(Trunk roads) ya kutoka Mikumi-Mahenge, Kilosa kwa mpepo-Londo ambopo
amesema kuwa Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya Kidatu –Ifakara(KM
67) kwa kiwango cha lami ifikapo machi mwakani wakati barabara ya Lupilo
hadi Lumecha upembuzi yakinifu unaendelea.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa halmashauri ya mji Ifakara Bw. Mashaka
Mbilinyi ameelezea umuhimu wa barabara hiyo kuwa itakuwa kichocheo cha
mendeleo ya kiuchumi kwa majimbo manne ya Mlimba, Malinyi, Ulanga na
Kilombero.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani (Wa
pili kulia), akiendelea na ukaguzi wa sehemu ya juu ya daraja la
Kilombero.
“Barabara
hii itakapokamilika itawawezesha wananchi kupata huduma katika sehemu
mbalimbali za majimbo yetu na pia kusafirisha kusafirisha mizigo ya
nafaka kwenda katika masoko mbalimbali na hivyo kukuza kipato cha
mwananchi na taifa kwa ujumla”. amesema Bw. Mbilinyi.
Naye
Mbunge wa Jimmbo la Mlimba Mhe. Suzani Kiwanga na Mbunge wa Kilombero
Mhe. Peter Lijuakali kwa pamoja wameishukuru Serikali na kusema kuwa
ujenzi wa barabara hiyo itakuwa mkombozi kwa wananchi wa kanda ya Kusini
kwa vile itaunganisha Kilombero, Malinyi na Ulanga na Mkoa wa Ruvuma.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani yupo
Mkoani Morogoro kwa ziara ya kukagua Miundombinu ya barabara, Madaraja
na Reli.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani (Wa
kwanza kushoto) akipata maelezo ya ramani ya Ujenzi wa Daraja la
Kilombero kutoka kwa Mkandarasi wa kampuni ya Rv associates India&
AES Tanzania. Daraja hilo lipo katika barabara kuu ya Ifakara –Mahenge
Mkoani Morogoro.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani
(aliyenyoosha kidole) akitoa maelekezo kwa Mkandarasi wa kampuni ya Rv
associates India&AES Tanzania anayejenga Daraja la Kilombero. Daraja
hilo lipo katika barabara kuu ya Ifakara –Mahenge Mkoani Morogoro.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani
(Mbele) akitoa akisisitiza jambo kwa Mkandarasi wa kampuni ya Rv
associates India& AES Tanzania anayejenga Daraja la Kilombero.
Daraja hilo lipo katika barabara kuu ya Ifakara –Mahenge Mkoani
Morogoro.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani (Wa
tatu kushoto) akifafanua jambo kwa Mkandarasi wa kampuni ya Rv
associates India&AES Tanzania anayejenga Daraja la Kilombero.Daraja
hilo lipo katika barabara kuu ya Ifakara –Mahenge Mkoani Morogoro.
Muonekano
wa Daraja la Kilombero lenye urefu wa Mita 384 ambapo ujenzi wake
unaendelea, Daraja hilo lipo katika barabara kuu ya Ifakara –Mahenge
Mkoani Morogoro.
Picha na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
No comments:
Post a Comment