Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Ndg. Athumani Kihamia akitoa taarifa fupi ya Jiji la Arusha kwa
Viongozi wa Huangshi China.
|
Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Mhe.
Kalisti Lazaro akiwakaribisha Viongozi kutoka Huangshi China wakati wa hafla ya
kusaini Mkataba wa Makubaliano.
|
Baadhi ya wataalamu walioshiriki katika
Hafla ya kusaini Mkataba wa Makubaliano.
|
Viongozi wa Jiji la Arusha wakisaini
Mkataba wa Makubaliano na Mji wa Huangshi- China.
|
Viongozi wa Huangshi – China wakisaini
mkataba wa Makubaliano na Jiji la Arusha.
|
Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Mhe.
Kalisti Lazaro (pili kulia) akimkabidhi Makamu Mwenyekiti wa Huangsh China
Mkataba wa Makubaliano ya kuanzisha Mji Dada.
|
Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha
akikabdihi zawadi kwa Makamu Mwenyekiti wa Huangshi-China.
|
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Ndg.
Athumani Kihamia akionyesha zawadi walizozipokea kutoka kwa viongozi wa
Huangshi-China walipotembelea Jiji la Arusha.
|
Katika Picha ya Pamoja Viongozi wa Jiji
la Arusha na Huangshi City baada ya kusaini Mkataba wa Makubaliano.
|
Halmashauri ya Jiji la Arusha mapema leo hii imesaini mkataba
na kufanya makabidhiano ya Mkataba wa Makubalino (MOU) na
baadhi viongozi wa Manispaa ya Huangshi – China waliotembelea Jiji hili kwa
lengo hilo.
Makubaliano hayo ya Mjidada
(Sistership) unalenga kuimarisha
urafiki baina ya Halmashauri ya Jiji la Arusha na Manispaa ya Huangshi, kubadilishana mbinu za kiutawala na kushirikiana katika nyanja mbalimbali
ikiwemo biashara na uchumi, Sayansi na Teknolojia pamoja na Elimu na utamaduni.
Akizungumza katika Hafla hiyo ya Utiaji Saini Mstahiki Meya
wa Jiji Mh. Kalisti Lazaro amesema huu ni mwanzo mzuri kwa Jiji la Arusha
kujitangaza katika Miji Mikubwa Duniani
inayoweza kutoa fursa kwa jamii ya watu
wa Arusha.
Naye Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Ndg. Athuman Kihamia alisisitiza kuwa Uhusiano huu utasaidia
kuimarisha mifumo ya kiutendaji katika maeneo yale ambayo Mji wa Huangshi
wamefanikiwa na hii itasaidia katika kutoa huduma bora kwa wananchi.
Kiongozi wa Msafara kutoka Huangshi ambaye pia ni Makamu
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Jumuiya wa watu wa Huangshi Bw. Wang Bin amesema Arusha ni Mji wa
kwanza Afrika kuingia nayo makubaliano ya kuanzisha Mji Dada na hii ni kwa
sababu ya mazingira rafiki ya uwekezaji yanayopatikana katika Jiji hili na
zaidi ukuaji wa Mji unaohamasisha biashara kufanyika wakati wote.
Halmashauri ya Jiji ina mahusiano na miji kumi na mbili
Duniani na kati ya hiyo Miji Minne iko katika Jamhuri ya watu wa China.
No comments:
Post a Comment