Pages

October 22, 2016

WAKRISTO OMBEENI AMANI YA TANZANIA NA DUNIA

ASKOFU Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amewataka Wakristo kuombea amani ya nchi na dunia kwa ujumla. 

Alitoa rai hiyo kabla ya kutoa baraka ikiwa ni baada ya kuzindua groto ya Bikira Maria na ambayo ni kanisa lililopo ofisi za Radio Maria Tanzania iliyopo Mikocheni, Dar es Salaam. 

Alisema waumini wana wajibu wa kuombea amani nchi na dunia kupitia Bikira Maria ambaye ni tumaini la amani. 

“Huyu Mama (Bikira Maria) ni chimbuko la neema, chimbuko la baraka na ni matumaini ya amani, si kwa taifa letu tu, lakini kwa ulimwengu mzima. Tumtembelee na tumuombe amani ya nchi na ulimwengu wote,” alisema. 

Pengo alisema ni imani yake waumini watatumia kanisa hilo kwa ajili ya sala na kuwa kamwe halitaachwa bure likiota vumbi na utando wa buibui. 

Awali, Rais wa Radio Maria Tanzania, Humphrey Kira alisema groto ya Bikira Maria imejengwa kwa miezi minne na kugharimu Sh milioni 118 na ina uwezo wa kuchukua watu 80 kwa wakati moja.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...