JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
TAWALA ZA
MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
|
||
|
||
|
Mkurugenzi wa Jiji
|
|
Simu:
Nukushi:
|
+255 27 2508073/2503494 (Director)
+255 27 2544330 (General)
+255 27 2545768
|
S. L. P. 3013,
20
Barabara ya Boma,
23101 ARUSHA,
Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz
Tovuti: www.arushacc.go.tz
|
|
||
|
|
|
UFAFANUZI
JUU YA TAARIFA YA UZUSHI ILIYOTOLEWA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII
Halmashauri
ya Jiji la Arusha inakanusha taarifa ya uzushi na upotoshaji iliyosambazwa
kwenye mitandao ya kijamii jioni ya leo tarehe 17.10.2016 ikimuhusisha
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Ndg. Athumani Kihamia pamoja na Mbunge wa Viti
Maalum Mkoa wa Arusha Mhe. Catherine Magige.
Taarifa hiyo
ya kughushi iliyochapishwa kwa kutumia nembo ya Jiji la Arusha imetengenezwa na
watu wenye nia ovu na dhamira mbaya kwa malengo ya kupunguza kasi ya utendaji wa
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Ndg.
Athumani Kihamia pamoja na Serikali Mkoani Arusha kwa ujumla.
Aidha taarifa
hiyo ya uzushi imebeba ujumbe wa kutunga wenye kusudio maalum la kumchonganisha
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha na mamlaka nyingine ikiwemo Mamlaka yake ya Uteuzi
ili kumchafulia jina na kumgombanisha na Mamlaka hiyo.
Halmashauri
ya Jiji la Arusha inaziomba Mamlaka zinazohusika na ufuatiliaji wa uhalifu wa
mitandao zikiwemo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) na Jeshi la Polisi
Nchini kufuatilia watu wote walioshiriki upotoshaji na uhalifu huo wa kimtandao
na kughushi ili kuwatia nguvuni na kuwachukulia hatua kali za Kisheria ili iwe
fundisho kwao na watu wengine wenye tabia ya aina hiyo.
Hata hivyo Halmashauri
ya Jiji la Arusha inapenda kuujulisha Umma kuwa, Mkurugenzi wa Jiji ataendelea kwa mujibu wa Sheria,
Taratibu na kanuni zilizopo kusimamia
maslahi ya Umma, kudhibiti mapato na matumizi ya Fedha za Umma ili kuhakikisha
maelekezo ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kutaka Fedha nyingi zitumike kwa
ajili ya shughuli za maendeleo na hasa kuwahudumia wanyonge inatekelezwa
ipasavyo. Pia Halmashauri ya Jiji inatoa wito kwa wadau wote ndani ya Jiji la
Arusha kuunga mkono jitihada hizo za kuwahudumia wanyonge.
Halmashauri
ya Jiji inapenda kuwaarifu watanzania wote kuipuuza mitandao inayotoa habari za
uzushi na kupuuza habari hiyo na nyinginezo za uzushi zinazoenezwa dhidi ya
viongozi kwani hazina ukweli wowote zaidi ya uchochezi na uchonganishi.
Aidha
Halmashauri ya Jiji la Arusha inawashauri wahusika wote wa uzushi huu kuacha
kupoteza muda badala yake waungane na Serikali katika utekelezaji wa Kauli Mbiu
ya HAPA KAZI TU.
Nteghenjwa Hosseah
Afisa Habari, Halmashauri ya Jiji
Arusha.
17 Oktoba,2016
No comments:
Post a Comment