Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea
Hati ya Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Ghana hapa nchini Kwame
Asamoah Tenkorang Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe
10 Oktoba, 2016 amepokea hati za utambulisho za mabalozi wanne
wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini.
Mabalozi
waliowasilisha hati zao za utambulisho Ikulu Jijini Dar es Salaam ni
Balozi wa Jamhuri ya Sudan hapa nchini Mhe. Mahjoub Ahmed Abd Allah
Sharfi, Balozi wa Jamhuri ya Slovakia hapa nchini Mhe. Frantisek
Dlhopolcek, Balozi wa Ukraine hapa nchini Mhe. Yevheni Tsymbaliuk na
Balozi wa Jamhuri ya Ghana Mhe. Kwame Asamoah Tenkorang.
Rais
Magufuli amezungumza na Mabalozi hao kwa nyakati tofauti baada ya
kupokea hati zao za utambulisho, ambapo wamesisitiza umuhimu wa
kuendeleza na kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na
nchi hizo kwa kujikita zaidi katika biashara na uwekezaji.
"Mhe.
Balozi najua nchi yenu ya Sudan ina utajiri wa mafuta na imefanikiwa
kujenga uchumi wake kupitia mafuta, sisi pia hapa nchini tumebaini uwepo
wa mafuta na gesi asilia katika maadhi ya maeneo, ningependa uhusiano
na ushirikiano wetu sasa ujielekeza katika kubadilishana uzoefu na ujuzi
wa namna tunavyoweza kunufaika na mafuta na gesi" amesema Rais Magufuli alipokuwa akizungumza na Balozi wa Sudani hapa nchini Mhe. Mahjoub Ahmed Abd Allah Sharfi.
Dkt.
Magufuli pia ametoa wito kwa wafanyabiashara na wawekezaji kutoka nchi
za Sudan, Slovakia, Ukraine na Ghana kuja kuwekeza hapa nchini katika
sekta mbalimbali zikiwemo Mafuta na gesi, Kilimo, Uvuvi, Mbuga za
wanyama, Madini na ufugaji.
"Hivi
sasa Tanzania ipo katika mpango wa ujenzi wa viwanda na pia
tunatekeleza mpango wa pili wa maendeleo, hivyo nakuomba Mhe. Balozi
uwahamasishe wafanyabiashara na wawekezaji wa Ukraine waje wawekeze
katika viwanda kwani soko la uhakika la bidhaa lipo" amesisitiza Dkt. Magufuli alipokuwa akizungumza na Balozi wa Ukraine hapa nchini Mhe. Yevheni Tsymbaliuk.
Aidha,
Rais Magufuli amewasihi Mabalozi wa Slovakia, Ukraine na Ghana ambao
makazi yao ya Ubalozi yapo Mjini Nairobi nchini Kenya kuanzisha Ubalozi
wao hapa nchini ili kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano katika
masuala ya biashara na uwekezaji.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
10 Oktoba, 2016.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru
Balozi mteule wa Ghana hapa nchini Kwame Asamoah Tenkorang mara baada
ya kupokea Hati yake za Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akijadiliana jambo na Balozi mteule wa Ghana hapa nchini Kwame Asamoah
Tenkorang Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea
Hati ya Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Jamhuri ya Sudan Mahjoub
Ahmed Abdallah Sharfi Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
katika picha ya pamoja na Balozi mteule wa Jamhuri ya Sudan hapa nchini
Mahjoub Ahmed Abdallah Sharfi mara baada ya kupokea Hati yake ya
utambilisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
na Balozi mteule wa Jamhuri ya Sudan hapa nchini Mahjoub Ahmed Abdallah
Sharfi mara baada ya kupokea Hati yake ya utambilisho Ikulu jijini Dar
es Salaam
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akijadiliana jambo na Balozi mteule wa Jamhuri ya Sudan hapa nchini
Mahjoub Ahmed Abdallah Sharfi mara baada ya kupokea Hati yake ya
Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiaagana
na Balozi mteule wa Jamhuri ya Sudan hapa nchini Mahjoub Ahmed Abdallah
Sharfi mara baada ya kupokea Hati yake ya Utambulisho Ikulu jijini Dar
es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea
Hati ya Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Ukraine hapa nchini
Yevhemsi Tsymbalik Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru
Balozi mteule wa Ukraine hapa nchini Yevhemsi Tsymbalik mara baada ya
kupokea Hati yake ya Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na
Balozi mteule wa Ukraine hapa nchini Yevhemsi Tsymbalik mara baada ya
kupokea Hati yake ya Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea
Hati ya Utambulisho kutoka kwa balozi mteule wa Jamhuri ya Slovakia
Frantisek Dlhopolcek Ikulu jijini Dar es Salaam
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru
balozi mteule wa Jamhuri ya Slovakia hapa nchini Frantisek Dlhopolcek
mara baada ya kupokea Hati yake ya Utambulisho Ikulu jijini Dar es
Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akijadiliana jambo na balozi mteule wa Jamhuri ya Slovakia hapa nchini
Frantisek Dlhopolcek mara baada ya kupokea Hati yake ya Utambulisho
Ikulu jijini Dar es Salaam.
Picha na Ikulu.
Picha na Ikulu.
No comments:
Post a Comment