Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo(tatu kulia) akisikiliza
mgogoro wa wananchi wa Samunge baada ya
wananchi hao kuzuia msafara wake.
|
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akienda kukagua eneo la
shule ya Msingi Samunge lililovamiwa na
Bw. Lemindi Njuda.
|
Mkuu wa Mkoa wa Arusha (pili kushoto) akionyeshwa mipaka ya eneo
la Shule ya Msingi Samunge na viongozi wa kijiji cha Samunge.
|
Wadau wa Habari katika picha ya pamoja na Babu wa Samunge
Mchungaji Ambilikile Mwasapila(pili kulia)
maarufu kama Babu wa Kikombe.
|
Babu wa Samunge Mch. Ambilikile Mwasapila (kushoto) akiwa na mdau
wa Habari. Babu wa Samunge ni miongoni mwa wananchi waliozuia Msafara wa Mkuu
wa Mkoa.
|
Nteghenjwa
Hosseah ,Loliondo
Migogoro ya ardhi katika wilaya ya
Ngorongoro Mkoani Arusha juzi iliingia katika sura mpya baada ya wananchi wa
kata ya Samunge wilayani humo akiwemo babu wa kikombe cha dawa, Mchungaji
Ambilikile Mwaisapile waliandamana na kufunga barabara na kuzuia msafara wa Mkuu wa Mkoa wa
Arusha Mrisho Gambo ili watatuliwe mgogoro wa ardhi ya shule iliyoporwa na
diwani mstaafu wa kata hiyo.
Wananchi hao wakiwa na mabango na
majani mabichi walizuia msafara huo ili waweze kusikililizwa kilio chao cha
muda mrefu baada ya baraza la kata kuamuru katika kesi yake aprill mwaka huu
kuwa ardhi hiyo ni mali ya shule lakini jeshi la polisi Ngorongoro limekuwa
likimlinda na kumkingia kifua mvamizi huyo na kukataa kutekeleza amri ya baraza
la ardhi kata iliyomtaka kuondoka katika eneo hilo la shule.
Baadhi ya mabango hayo yalikuwa
yakisomeka '' tumeporwa ardhi yetu Mkuu wa Mkoa tusaidie'' lingine likisema
''wenye fedha wamepora ardhi ya shule na polisi inawalinda na kuwakingia
kifua'' na bango lingine lililosomeka ''Mkuu wa Mkoa tunaomba ushuke
utusikilize viongozi wa wilaya wote wamenunuliwa''
Kabla ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha kuteremka
kuwasikiliza aliteremka Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Rashid Taka na Mkuu wa
polisi wa wilaya hiyo OCD Warioba kwa lengo la kuwatuliza na kuwasihii kuacha
mukari ili waeleza kero zao kwa utulivu na amani bila ya vurugu zozote.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa
kata hiyo, Mtendaji wa kata hiyo Zakaria Antony alisema kuwa eneo hilo lenye
ukubwa wa ekari 15 limeporwa na mfanyabiashara na diwani mstaafu Lemindi
Njuda ambaye amefanya kilimo cha migomba na shughuli nyingine za kijamii.
Antony alisema kuwa uamuzi wa
kuondolewa kwa diwani huyo wa zamani katika eneo la shule ulitolewa na baraza
la ardhi kata aprill mwaka huu lakini jeshi la polisi wilaya ya Ngorongoro
limekuwa likimlinda na kugoma kutekeleza amri baraza na badala yake limeandika
barua ya kutobugudhiwa katika shamba hilo na hatua kali zinachukuliwa kwa
mwananchi atayekiuka amri hiyo.
Mtendaji huyo aliendelea kusema kuwa
wananchi wanashindwa kufanya shughuli za maendeleo hususani ujenzi wa madarasa
na nyumba za walimu kutokana na ufinyu wa eneo la shule hivyo walimuomba Mkuu
wa Mkoa kusaidia mgogoro huo ili haki iweze kutendeka kwani polisi imewekwa
mfukoni na tajiri huyo.
Naye Mchungaji Ambilikile Mwaisapile
alisema kuwa yeye yuko mstari wa mbele kuhakikisha shule inarudishiwa eneo lake
lililoporwa na watu wenye fedha na nguvu za ushawishi kwani mungu hapendi vitu
vya dhuruma.
Mchungaji alisema yeye pamoja na wananchi
wa kata hiyo walikuwa wakisaka haki kila ofisi ya wilaya ya Ngorongoro lakini
haki hiyo walishindwa kuipata kutokana na mapokezi mabovu ya viongozi wa
serikari wilaya ya Ngorongoro.
Mkuu wa Mkoa Gambo kwa alimwamurisha
OCD kufuta nakala ya barua aliyoandika mkuu wake wa kituo cha polisi Loliondo
kwani yeye hana mamlaka ya kufanya hivyo bali anapaswa kutekeleza amri ya
mahakama ya baraza la kata na sio vinginevyo.
Gambo pia alimwagiza Mkuu wa wilaya ya
Ngorongoro pamoja na kamati yake ya ulinzi na usalama kuhakikisha wanasimamia
kikamilifu utekelezaji wa amri hiyo ili shughuli za maendeleo ya shule hiyo
ziweze kufanyika mara moja.
Alisema na kusikitishwa kuona wananchi
wana kero ya kutaka maendeleo lakini viongozi wa serikali kwa kujali matumbo
yao na kuendekeza rushwa wako mstari wa mbele kuzuia wananchi kufanya
shughuli za ujenzi wa shule.
Pia Mkuu huyo aliwataka viongozi wa
wilaya kumaliza mgogoro mwingine wa ardhi uliopo karibu na zahanati ya kata
hiyo ili wananchi waweze kufanya shughuli nyingine za maendeleo na kuacha
kukesha kufikiria migogoro ya ardhi kila kukicha ambayo mingi inasababishwa na
viongozi.
Baada ya maelezo hayo wananchi
walionyeshwa kufurahishwa na uamuzi huo na kuahidi kutoa ushirikiano wa hali na
mali katika shughuli za maendeleo.
No comments:
Post a Comment