Pages

October 6, 2016

MKUTANO MKUU WA WANACHAMA WA MUUNGANO WA KLABU ZA WAANDISHI WA HABARI NCHINI UTPC WAANZA JIJINI MWANZA

Rais wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini UTPC, Deo Nsokolo, akifungua Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini UTPC unaofanyika Jijini Mwanza kwa siku mbili, kuanzia leo Oktoba 06,2016.

Mkutano huo unajadili masuala mbalimbali ikiwemo Mpango Mkakati wa UTPC kwa mwaka 2016/20 uliofadhiriwa na Shirika la Sida.
Na BMG
Viongozi wa UTPC wakiwa kwenye mkutano huo ambapo kutoka kulia ni Mkurugenzi wa UTPC, Abubakar Karsan, Rais wa UTPC, Deo Nsokolo, Makamu wa Rais wa UTPC, Jane Mihanji na Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili UTPC
Wajumbe wa bodi, UTPC, wakiwa kwenye mkutano huo
Mwenyekiti wa Mara Press Club, Mugini Jacob (kulia) akiwa na wajumbe wengine kwenye Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini UTPC
Mwenyekiti wa Mara Press Club, Mugini Jacob (kushoto) akiwa na wajumbe wengine kwenye Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini UTPC
Wajumbe mbalimbali wakiwa kwenye Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini UTPC
Mweka Hazina Mara Press Club akichangia jambo kwenye mkutano huo
Wajumbe mbalimbali wakiwa kwenye Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini UTPC
Wajumbe mbalimbali wakiwa kwenye Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini UTPC
Wajumbe mbalimbali wakiwa kwenye Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini UTPC
Wajumbe mbalimbali wakiwa kwenye Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini UTPC
Wajumbe mbalimbali wakiwa kwenye Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini UTPC
Mwenyekiti wa Mara Press Club, Mugini Jacob (kulia) akisalimiana na Rais wa UTPC, Deo Nsokolo (kushoto) kwenye mkutano huo
Mwenyekiti wa Mara Press Club, Mugini Jacob (kulia) akisalimiana na Makamu wa Rais wa UTPC, Jane Mihanji (kushoto) kwenye mkutano huo
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoani Shinyanga, Kadama Malunde (kulia) akisalimiana na Rais wa UTPC, Deo Nsokolo (kushoto).
*****************************************x
Waandishi wa Habari nchini wametakiwa kuusoma na kuuelewa vyema mswada sheria ya huduma ya vyombo vya habari 2016, uliowasilishwa na Serikali bungeni mjini Dodoma, kwa ajili ya kutoa maoni yao juu ya mswada huo.

Rais wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini UTPC, Deo Nsokolo, ameyasema hayo kwenye Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Muungano huo, unaofanyika kwa siku mbili Jijini Mwanza kuanzia leo.

Nsokolo amesema tayari kamati ya bunge imekwisha kabidhiwa mswada huo kwa ajili ya kukusanya maon hivyo ni vyema waandishi wa habari ambao wanaguswa moja kwa moja na mswada huo, wakausoma kiundani na kisha kutoa maoni yao kabla ya kuwasilishwa bungeni ili kuidhinishwa.

Akiwasilisha mswada huo katika bunge lililopita, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, alisema ikiwa mswada huo utapitishwa na bunge kuwa sheria, utasaidia kuleta mageuzi makubwa ya kitaaluma kwa wanahabari pamoja na huduma za vyombo vya habari nchini.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...