Burudani nayo ilikua sehemu ya kunogesha Nyerere Day
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
TAWALA ZA
MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
|
|
Barua zote zitumwe
kwa:
|
Mkurugenzi wa Jiji
|
Simu:
Nukushi:
|
+255 27 2508073/2503494 (Director)
+255 27 2544330 (General)
+255 27 2545768
|
S. L. P. 3013,
20
Barabara ya Boma,
23101 ARUSHA,
Tovuti: www.arushacc.go.tz
|
Unapojibu tafadhali
taja:
TAARIFA KWA VYOMBO YA HABARI
|
|
|
|
|
|
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arusha kwa kushirikiana
na wadau wa michezo pamoja na wananchi wa Jiji wameadhimisha siku ya Mwl.
Nyerere kwa kuandaa na kushiriki kwenye Bonanza la Michezo lililopewa Jina la
Bonaza la Mwalimu Nyerere lililofanyika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid uliopo jijini hapa leo tarehe
14.10.2016.
Tamasha hili limeandaliwa maalumu kwa ajili ya kumuenzi baba
wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyenyere aliyefariki miaka kumi na saba iliyopita
sambamba na kusherekea kilele cha Mwenge wa Uhuru ambao ulipita katika Wilaya ya
Arusha mwishoni mwa mwezi wa nane na kuzindua miradi ya Afya, Maji, Elimu,
Uwezeshaji wananchi, uwezeshaji makundi maalumu, Ujenzi na Usafi wa Mazingira yenye
thamani ya zaidi ya TshBil 1.5.
Akiongea na wanamichezo walioshiriki katika Bonanza hilo Mkuu
wa Wilaya ya Arusa Mhe. Gabriel Fabian
Daqarro alisema Tamasha hili ni kwa ajili ya kumuezi Mwl. Nyenyere ambapo litasaidia
vijana na wananchi kuweka miili yao safi, kujiepusha na maradhi pamoja na makundi
yanayoweza kusababisha kujiingiza kwenye madawa ya kulevya, ulevi na uzururaji.
Pia tuitumie siku hii kutafakari mafundisho na maelekezo ya Mwalimu
Nyerere aliyoyatoa wakati wa uhai wake, wapi Nchi imetoka, Misingi imara ya Uongozi
bora na namna gani tunaweza kuenenda ili kuleta maendeleo katika Taifa letu, na
vijana kama nyie ndio mnaotakiwa kuwa chachu katika kupambana na umasikini
katika Nchi yetu alisema Dc Daqarro.
Naye Katibu Tawala wa Wilaya ya
Arusha Bw. David Mwakiposa alielezea
Tamasha hilo kuwa limeshirikisha michezo mbalimbali kama Netball, Football,
Volleyball, Basketball, mchezo wa Bao, kukimbiza kuku, Baiskel, kuvuta kamba, Karate,
Taekondo, Uchoraji pamoja na riadha.
Bonaza hili pia limetumika kama jukwaa la kuendelea kuelimisha
na kueneza ujumbe kwa vijana kupitia kauli mbiu ya Mwenge mwaka 2016 inayosema
“Vijana ni nguvu kazi ya Taifa washirikishwe na wawezeshwe”.
Nteghenjwa Hosseah
Afisa Habari, Halmashauri ya Jiji
Arusha
14.10.2016
|
No comments:
Post a Comment