Bilionea wa 21 Afrika na mkurugenzi mtendaji mkuu wa makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL) Mohammed Dewji ambaye ana dhamira ya kununua asilimia 51 yaa hisa za Simba kwa Tsh Bilioni 20, ametekeleza ahadi yake ya kuchangia mfuko wa usajili wa Simba kwa kutoa Tsh milioni 100 kwa Rais wa SimbaEvans Aveva.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri katika mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari Mohammed Dewji alipotangaza mpango wake wa kununua hisa Simba, alisema kama mkutano mkuu wa Simba uliofanyika Julya 31 2016 wakikubali mfumo wa mabadiliko ya utawala na klabu ikaendeshwa kwa mfumo wa hisa, atasaidia mfuko wa usajili wa Simba.
August 2 2016 mbele ya waandishi wa habari katibu mkuu wa Simba Patrick Kahemelena Rais wa Simba Evans Aveva, Dewji amekabidhi hundi ya Tsh Milioni 100 kama sehemu ya kutimiza ahadi yake, kati ya zaidi Tsh Milioni 400 ambazo ni bajeti ya usajili yaSimba msimu huu, akiuziwa asilimia 51 ya hisa Simba Dewji ameahidi bajeti ya usajili yaSimba itakuwa zaidi ya Tsh Bilioni 1.
No comments:
Post a Comment