![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhU8Ho545q2W8VgF-Mf-lMynJ-RhZMO9tV8iKvTrQZEY2UmEyOmItZz0cXgXq2dWdUMPU69lCAx7tYl5-zfniL2t06lzkZmzzCxQG58lCEIQD7PJQM-V0YJGr3YE0pJG9PVESmiJM7IaZs/s640/parade.jpg)
Baadhi
ya maofisa na Wanamichezo wa Michezo ya majeshi kwa Nchi za Afrika
Mashariki wakifuatilia Ufunguzi wa Michuano hiyo uliofanyika katika
Uwanja wa Amahoro Kigali Nchini Rwanda
Baadhi
ya maofisa na Wanamichezo wa Michezo ya majeshi kwa Nchi za Afrika
Mashariki wakifuatilia Ufunguzi wa Michuano hiyo uliofanyika katika
Uwanja wa Amahoro Kigali Nchini Rwanda
Waziri
wa Ulinzi wa Rwanda Jenerali James kabarebe (wa pili Kulia) akifuatilia
jambo wakati wa ufunguzi wa Michuano ya majeshi kwa nchi za Afrika
mashariki katika Uwanja wa Amahoro Kigali nchini Rwanda
Wanarianda
walioshiriki mashindano ya majeshi kwa nchi za Afrika mashariki
wakichuana wakati wa Mashindano hayo kwa Mbio za nyika Wanawake ambapo
Tanzania imeshika nafasi ya Tatu.
(picha na Selemani Semunyu)
Na Seleamani Semunyu JWTZ.
MASHINDANO
ya majeshi kwa Nchi za Afrika mashariki yameingia Siku yake ya kwanza
baada ya kuzinduliwa huku Tanzania ikishika nafasi ya tatu katika Riadha
kwa wanawake katika mbio zilizokuwa na Ushindani Mkali na kufanyika
katika Uwanja wa APRC Kicukiro. .
Mtanzania
Catherine Lange aliiwezesha Timu ya JWTZ kuibuka na Ushindi wa tatu
huku kwa Wanaume Mwanariadha Fabiano Nelson kufanya vyema licha kukosa
ushindi wa jumla kutokana na kuwa peke yake mbele nyuma ya wakenya
waliochukua ushindi wa Kwanza.
Awali
akifungua mashindano hayo Waziri wa Ulinzi wa Rwanda Jenerali James
Kabarebe amewapongeza Wakuu wa Majeshi Kutoka Nchi za Afrika Mashariki
kwa kuendeleza michezo na kutoa nafasi kwa nchi zo kushiriki katika
mashindano ya Afrika Mashariki ambayo yamekuwa kiungo katika kuimarisha
Ushirikiano.
Aliyasema
hayo leo wakati akizindua wa michezo hiyo katika Sherehe zilizofanyika
katika Uwanja wa Amahoro Kigali Nchini Rwanda na Kuhudhuriwa na Viongozi
mbalimbali wa Majeshi kutoka majeshi ya Nchi Nne zinazoshiriki
Michuano hiyo.
“
Michezo ni Sehemu ya Majukumu ya Jeshi Lakini nawapongeza na kuyapa
uzito mashindano haya kwani yamekuwa yakitusaidia katika kuimarisha
ushirikiano wa Nchi hizo ili kuhakikishia inaendelea kuwa sehemu salama.
Waziri
Jenerali Kabarege alitoa Wito kwa Wakuu hao kutumia nafasi ya Michezo
hii kufanyia kazi changamoto kama zipo zinazokabili majeshi katika
ukanda huu.
Awali
Mkuu wa majeshi wa Rwanda Jenerali Patrick Nyamvumba aliwahahakikishia
Wanamichezo maandalizi Mazuri na kuwataka kuwa huru na kuchanganyika na
Wanyarwanda ambao alidai wameajiandaa kuwapokea.
Kwa
upande wake Mwakilishi wa Mkuu wa majeshi ya Ulinzi wa Tanzania ambaye
ni Mkuu wa mafunzo na Utendaji Kivita Meja Jenerali Issa Nassoro amesema
anamatumaini makubwa kwa Timu za Tanzania kurejea na vikombe.
No comments:
Post a Comment