Pages

August 6, 2016

LHRC YAMPA MAPOKEZI MAKUBWA MWANAHARAKATI GELINE FUKO AKITOKEA MAREKANI



Geline Fuko (kushoto) akipokea maua kutoka kwa wafanyakazi wenzake wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC),ikiwa ni ishara ya kumpongeza baada ya kutua  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam jana, akitokea Marekani alikokuwa akihudhuria mafunzo ya vijana wa kiafrika yaliyoandaliwa na

Raisi Obama.


Na Dotto Mwaibale

SHANGWE ilitawala wakati mtanzania Geline Fuko alipo wasili Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) majira ya saa nne usiku jana Agosti 5, 2016 akitokea nchini Marekani alikohudhuria mafunzo ya viongozi vijana kutoka Bara la Afrika. 

Wafanyakaziwa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu ambao ni wafanyakazi wenzake wa Geline, familia ya Geline, ndugu na marafiki walitoa mapokezi ya kishujaa wa wanaharakati huyo aliyetajwa kuwa mfano wa kuigwa na Rais Obama.


Akizungumza na wanahabari, Geline alisema amefarijika na hakutarajia kama wazo lake la kuanzishwa kwa Kanzidata ya Katiba litakuwa wazo kubwa  ambalolitakubalika mpaka na Rais Obama. 

Hata hivyo Geline alisema amefurahishwa na program hiyo ya Mandela Washington Fellowship kwani imewawezesha washiri kikujifunza mambo mengi na  kupata uono mpana zaidi wakufanya mambo.

Geline iliwahimiza watanzania kutembelea Kanzidata hiyo iliyopo mtandaoni (http://katiba.humanrights.or.tz/) ili kuweza kuijua katiba yao na kuweza kujua haki zao kama watanzania. 

Mwisho alishukuru wa mapokezi makubwa ambayo pia hakuyatarajia.

Akitoa neno la shukurani kwa Geline kwa niaba ya LHRC, Mkurugenzi wa Fedha naUtawala-LHRC, Ezekiel Masanja amempongeza Geline kwa kuitoa kimasomaso LHRC na Tanzania kwa ujumla.

Geline Fuko amepata kutambulika baada ya Rais Obama kumtaja kama mfano wa kuigwa wa wanaharakati wa haki za binadamu wakati akizungumza Jumatano Agosti 3, 2016 katika kilele cha mpango wake wa kuwawezesha vijana wakiafrika unaojulikana kama Mandela Washington Fellowship. 

Raisi Obama alimsifu mwanasheria huyo kutoka LHRC ambaye ni moja  ya vijana 1000 waliokuwa jijini Washington kwa lengo la kujengewa uwezo ili kuweza kusaidia Maendeleo katika Nyanja zote za maisha katika nchi zao.

RaisiObamaalisifujuhudizaGelinezakuibuawazo la kuanzishakwamaraya kwanza Kanzidata ya Katiba nchini Tanzania kwa kutekeleza wazo hilo chiniya LHRC. 

Raisi Obama alikaririwa akisema Marekani itaendelea kushikamana na wanaharakati kama Geline Fuko kutoka Tanzania. 

GelinenimwanasherianamwanaharakatiwahakizabinadamuambayeamefanikishakuanzishwakwaKanzidatayaKatibaya kwanza nayapekeenchini Tanzania inayowawezesha watanzania kusoma Katiba kupitia simu zao za mkononi”.

Programu ya Mandela Washington Fellowship yenye lengo la kuwa wezesha vijana wa Kiafrika katika Nyanja za kiuchumi, kisiasa, kiteknolojia na kijamii ilianzishwa na Rais Obama mwaka 2014. 

Programu hii hujumuisha vijana elfu moja (1000) kutoka nchi mbalimbali za Afrika ambao hugharamiwa na serikali ya Marekani kwenda jijini Washington kwa lengo la kujengewa uwezo zaidi.


Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kilianzisha Kanzidata ya Katiba mwaka mmoja uliopita mnamo Julai 15, 2015. 

Kupitia tovuti maalumu (http://katiba.humanrights.or.tz/) na simu za mkononi, watanzania wanaweza kusoma Katiba katika Kanzidata hiyo.

(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...