Wajumbe wa Bunge la Korea Kusini wakiwa katika picha ya pamoja na
baadhi ya viongozi na watumishi wa Shirika la Hifadhhi za Taifa (TANAPA )
na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Na Dixon Busagaga Globu ya Jamii, Kanda ya Kaskazini.
Hifadhi
ya Taifa ya Serengeti kwa kushirikiana na serikali ya Korea ya
Kusini imeanza mchakato wa ujenzi wa kituo cha kimataifa cha kutunza
taarifa za mienendo ya Wanyamapori kitakachojulikana kama Serengeti
Internatinal Media Centre.
Kituo hicho kinachotarajiwa kugharimu zaidi shilingi bilioni nne kitajengwa katika Hifahi ya Taifa ya Serengeti .
Tayari
serikali ya Korea Kusini imeshatuma wajumbe wake kuja nchini
tanzania kujionea eneo kitakapojengwa kituo hicho na kukamilisha
taratibu nyingine muhimu ambapo kiongozi wa wajumbe hao Park Joosung
amesema mradi huo ni mwendelezo wa ushirikiano wa Korea Kusini na
Tanzania katika kuimarisha uhifadhi.
Akizungumza
na ujumbe huo mkuu wa hifadhi ya taifa ya serengeti Wiliam
Mwakilema amesema kituo hicho kikikamilika kitaongeza chachu utalii na
kitatoa fursa kwa wageni kuona aina nyingi zaidi za wanyama.
Naye
mratibu wa ujenzi bw Victor Ketance amesema ujenzi utaanza mwezi
october mwaka huu na unatarajiwa kumalizika baada ya miezi 14.
Wajumbe
wa Kamati ya Maendeleo kwa Afrika katika Bnge la Korea Kusini
wakiwasili katika uwanja mdogo wa ndege uliopo katika Hifadhi ya Taifa
ya Serengeti.
Meneja
Masoko wa Shirika la Hifadhi za Taifa,TANAPA,Victor Ketance akipokea
ugeni wa wajumbe kutoka Bunge la Korea Kusini walipotembelea Hifadhi ya
Taifa ya Serengeti kwa ajili ya kutizama eneo la uwekezaji wa kituo cha
kisasa cha taarifa za hifadhi hiyo.
Mkuu
wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (SENAPA) William Mwakilema akipokea
ugeni wa wajumbe kutoka Bunge la Korea Kusini walipotembelea Hifadhi ya
Taifa ya Serengeti kwa ajili ya kutizama eneo la uwekezaji wa kituo cha
kisasa cha taarifa za hifadhi hiyo.
Mkuu
wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (SENAPA) William Mwakilema
akisalimiana na wadau wa utalii,Zainabu Ansel ,Mkurugenzi wa kampuni ya
Utalii ya Zara(katikati) na Mkurugenzi wa Kibo Safari's Willy
Chamburo.(kushoto) waliokuwepo uwanjani hapo.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Kibo Safari's ,Willy Chamburo (katikati) akizungumza
jambo na kiongozi wa ugeni wa Korea Kusini Won Yul Chui (kushoto) baada
ya kukutana katika uwanja mdogo wa ndege uliopo Hifadhi ya Taifa ya
Serengeti .kulia ni Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti
William Mwakilema.
Wajumbe
wa Kamati ya Maendeleo ya Afrika katika Bunge la Korea Kusini wakitia
saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Hifadhi ya
Taifa ya Serengeti kwa ajili ya kuangalia eneo lililotengwa kwa ajili ya
ujenzi wa kituo cha kisasa cha taarifa za hifadhi hiyo.
Mhifadhi
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ,William Mwakilema (kushoto)
akizungumza na Wajumbe wa kamati ya Maendeleoo ya Afrika ya Bunge la
Korea Kusini waliofika katika Hifadhi hiyo kwa ajili ya ufuatiliaji wa
maenedeleo ya kuanza kwa mradi wa ujenzi wa kituo cha kisasa cha Taarifa
katika Hifadhi hiyo.
Mhifadhi
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti,William Mwakilema akiongoza
Ujumbe wa Wabunge wa Bunge la Korea Kusini walioko katika kamati ya
Maendeleo ya Afrika kutembelea maeneo kutakapo jengwa kituo cha kisasa
cha taarifa.
Ujumbe
wa Wabunge wa Bunge la Korea Kusini wakitizama picha ya Hayati Baba wa
Taifa ,Mwl Julius K. Nyerere akiwa na rafiki yake Prof,Dkt Bernhard
Grzimek huku wakipata maelezo kutoka kwa Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya
Taifa ya Serengeti ,William Mwakilema.
Ujumbe
wa Wabunge wa Bunge la Korea Kusini wakipata maelezo katika michoro ya
kituo cha kisasa cha taarifa katika Hifadhi ya taifa ya Serengeti.
Mhifadhi
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ,William Mwakilema akitoa zawadi
kwa wajumbe wa Bunge la Korea Kusini mara baada ya kutembelea eneo
kutakapo jengwa kituo cha kisasa cha taarifa katika hifadhi hiyo.
No comments:
Post a Comment