Pages

August 28, 2016

JWTZ KUADHIMISHA MIAKA 52 SEPTEMBA MOSI 2016 KWA KUFANYA USAFI NCHI NZIMA


Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) limepanga kuadhimisha miaka 52 ya kuanzishwa kwake, kwa kufanya usafi katika maeneo mbalimbali, siku ya maadhimisho hayo Septemba Mosi, 2016.
Habari iliyorushwa na mtandao wa Dar24, imemnukuu msemaji wa JWTZ Kanali Ngemela Lubinga akisema kuwa Jeshi hilo litasherehekea bila kufanya maandamano ya aina yoyote na kwamba linafahamu kuwa Serikali imeshapiga marufuku maandamano siku hiyo.
“Ratiba yetu ni kusherehekea, tunajua serikali imeshapiga marufuku maandamano, lakini sisi kama wanajeshi tutafanya shughuli zetu kamazilivyopangwa”, alisema Lubinga.
JWTZ liliundwa Septemba Mwana 2064baada ya kuvunjwa rasmi kwa jeshi lilorithiwa kutokakwa wakoloni la Tanganyika Rifles.
Taamko hilo la JWTZ imekuja wakati ambapo kumekuwepo na mvutano wa kufanyika akwa maanadamano ya Operesheni ya UKUTA iliyoandaliwa na Chama cha CHADEMA ambayo serikali imeyapiga marufuku.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...