Wanavikundi 30 kutoka Kata za Jiji la Arusha walionufaika na mikopo iliyotolewa na Halmashauri ya jiji hilo yenye thamani ya Sh 403 milioni kuwawezesha wananchi kujiajiri. |
Arusha.Halmashauri ya Jiji la Arusha imetoa mikopo yenye thamani ya Sh 405 Milioni kwa vikundi 30 vya Wanawake na Vijana ikiwa utekelezaji wa kanuni ya kutenga asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa makundi hayo.
Akizungumza
wakati akikabidhi hundi kwa vikundi vilivyonufaika ,Mstahiki Meya
wa Jiji la Arusha,Kalist Lazaro alisema kuwa fedha hizo zitumike kwa
malengo yaliyokusudiwa ili kuwawezesha wananchi wengine kukopa.
"Hizi
fedha sio sadaka ni mikopo ambayo mnatakiwa kuzirejesha kwa riba ya
asilimia 10 tu pekee ambayo huwezi kuipata sehemu nyingine hivyo ni
imani yangu kuwa mtarejesha kwa wakati kupitia vikundi mama yaani Saccos
na Vicoba kwenye Kata zenu,"alisema Kalist
Alisema
vikundi vitakavyorejesha kwa wakati vitafikiriwa kukopeshwa fedha tena
na kuongezewa kiwango na vitakavyoshindwa hatua za kisheria
zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kunyimwa mikopo hiyo katika Kata
husika.
Naye
Naibu Meya wa jiji,Viola Lindikikoki alisema mikopo hiyo inatolewa
bila kujali itikadi za vyama vya siasa au namna nyingine yeyote kwani
maendeleo ni kwaajili ya wananchi wote na wamejipanga kuwatumikia.
Alisema
mikopo kwa vikundi itakua ikitolewa kila baada ya miezi mitatu badala
ya mara moja kwa mwaka hivyo kuwataka wanawake na vijana kubuni miradi
itakayowaingizia kipato kwa kujishughulisha katika ujasiriamali.
Jiji
la Arusha lina jumla ya vikundi vya vijana 132 na vikundi vya wanawake
263 na kila mwaka wa fedha hupatiwa mikopo yenye masharti nafuu huku
mwaka 2013/14 halmashauri ilitoa mikopo yenye thamani ya Sh 194 milioni
na mwaka 2014/15 vikundi vilipokea kiasi cha Sh 13 milioni.
No comments:
Post a Comment