Pages

July 29, 2016

WAZIRI MAHIGA AAGANA NA MABALOZI WALIOMALIZA MUDA WA UWAKILISHI NCHINI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Balozi wa Uingereza hapa nchini, Mhe. Dianna Melrose alipokuja Wizarani kumuaga mara baada ya kumaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini. Katika mazungumzo yao Waziri Mahiga alimpongeza Balozi Melrose kwa kuiwakilisha nchini yake vema na kuendeleza mahusiano mazuri kati ya Tanzania na Uingereza. Kwa upande wa Balozi Melrose, alisema anaishukuru Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Serikali kwa ujumla kwa ushirikiano aliokuwa anaupata kipindi chote cha uwakilishi wake. 
Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine(wa kwanza kushoto) pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga (wa kwanza kulia) na Afisa Mambo ya Nje, Bi. Mona Mahecha nao wakifuatilia kwa makini mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea. 
Mazungumzo yakiendelea 

Wakati huo huo Mhe. Waziri Mahiga alikutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Canada nchini. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Balozi wa Canada nchini, Mhe Alexandre Leveque alipokuja Wizarani kumuaga mara baada ya kumaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini. Mhe. Mahiga alimpongeza na kumshukuru kwa kuendelea kushirikiana na Tanzania katika sekta mbalimbali zikiwemo Elimu na Biashara. Pia Mhe . Alexandre Leveque alitumia fursa hiyo kuishukuru Wizara kwa ushirikiano katika kipindi chake chote cha uwakilishi hapa nchini. 
Mkurugenzi wa Idara ya Amerika na Ulaya Balozi Joseph Sokoine(wa kwanza kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga (wa kwanza kulia) na Afisa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Lilian Kimaro wakifuatilia mazungumzo hayo kwa makini. 
Balozi Mahiga akiagana na Balozi Leveque mara baada ya kumaliza mazungumzo 
.... Mazungumzo na Balozi wa Ireland hapa nchini 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Balozi wa Ireland nchini, Mhe. Fionnuala Gilsenan alipokuja Wizarani kuaga mara baada ya kumaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini. Mhe. Mahiga alimpongeza na kumshukuru kwa kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Ireland katika sekta mbalimbali. Kwa upande wa Mhe. Gilsenan alitumia fursa hiyo kuishukuru Wizara na Serikali kwa ujumla kwa ushirikiano.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...