Meneja
Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete
akitoa neno la ukaribisho kwa wanahabari na wageni wengine katika hafla
fupi ya kukabidhi hundi kwa wanariadha wanaounda timu ya taifa,
inayojiandaa na mashindano ya Olimpiki yatakayoafanyika mwezi Agosti
nchini Brazil.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi,akizungumza
wakati wa hafla fupi ya kukabidhi hundi ya Shilingi Milioni tano kwa
wanariadha wanaounda timu ya taifa inayojiandaa na mashindano ya
Olimpiki.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi akikabidhi
mfano wa hundi ya Shilingi Milioni tano kwa Rais wa Shirikisho la Riadha
Tanzania (RT) Anthony Mtaka kwa ajili ya kusaidia wanariadha wanaounda
timu ya taifa wakijiandaa na mashindano ya Olimpiki.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi
akikabidhi "Track Suit "maalumu zenye maandishi na nembo yanayotangaza
vivutio vya utalii vilivyopo nchini kwa Rais wa Shirikisho la
Riadha Tanzania (RT) Anthony Mtaka kwa ajili ya kusaidia wanariadha
wanaounda timu ya taifa wanaojiandaa na mashindano ya Olimpiki
Rais
wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Anthony Mtaka akizungumza mara
baada ya kukabidhiwa hundi pamoja na mavazi maalumu kwa ajili ya
wanariadha hao .
Baadhi
ya viongozi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) waliohudhuria hafla
hiyo.kutoka kushoto Mkurugenzi wa Utalii na Masoko,Ibtahim Musa,Meneja
Utalii Johnson Manase na Mhifadhi Vitalis Uruka.
Wanariadha
watakaoiwakilisha nchi katika mashindano ya Olimpiki katika jiji la Reo
De Jeneiro nchini Brazil wakiwa katika mavazi maalumu yanaotangaza
vivutio vilivyoko nchini.
Mkufunzi wa Wanariadha wanaojiandaa na mashindano ya Olyimpiki ,Francis John akizungumzia matarajio yake juu ya vijana hao.
Baadhi
ya Wanahabari na wageni wengine waliofika katika ofisi za Makao Makuu
ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kushuhudia makabidhiano hayo.
Mwanariadha Said Makuka atakayepeperusha bendera ya Tanzania katika michuano ya Olyimpiki nchini Brazil.
Mwanariadha Sara Ramadhan ,mwanadada pekee atakayepeperusha bendera ya Tanzania katika michuano ya Olyimpiki nchini Brazil.
Mwanariadha Alphonce Felix atakayepeperusha bendera ya Tanzania katika michuano ya Olyimpiki nchini Brazil.
Mwanariadha Fabian Joseph atakayepeperusha bendera ya Tanzania katika michuano ya Olyimpiki nchini Brazil.
Wanariadha
wanne watakao iwakilisha Tanzania katika Michuano ya Olyimpiki nchini
Brazil wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi pamoja na Rais wa Shirikisho la
Riadha Tanzania (RT) Antony Mtaka ,wengine kutoka kulia ni Mkufunzi wa
wanariadha hao,Francis John na anyefuatia ni Mkurugenzi wa Utalii na
Masokowa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Ibrahim Musa.
Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog,Kanda ya Kaskazini.
SHIRIKA la Hifadhi
za Taifa (TANAPA) limetangaza kutumia
fursa ya mashindano ya Olyimpiki yanayotarajia kuanza mwezi ujao katika jiji la
Rio de Janeiro nchini Brazili kutangaza vivutio vya utalii kupitia wanariadha
wa Tanzania.
Hadi sasa ni
wanariadha wanne ,wakiume watatu na wa kike mmoja ndio waliofuzu kushiriki
mashindano hayo na tayari wako kambini katika hosteli za Chuo cha Misitu cha
FITI zilizoko West Kilimanjaro wilayani Siha.
Akiongea mjini Arusha wakati akikabidhi msaada wa fedha
na vifaa kwa ajili ya wanariadha hao Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA,Allan Kijazi amesema
wameamua kutumia fursa hiyo pia kusaidia wanariadha hao wanaoiwakilisha nchi
katika mashindano hayo ili waweze kurejea na medali.
Akishukuru kwa
msaada huo Rais wa Shirikisho la Riadha nchini ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu AnthonY Mtaka amesema fedha hizo zitatumika kwa ajili ya kuwakatia bima
ya Afya mwaka mmoja wanariadha hao pamoja na familia zao ili wanapokua nchini
Brazili wasiwe na mawazo mengi kuhusiana na familia zao walizoziacha hapa
nchini.
Naye mmoja wa
wanariadha waliofuzu kushiriki mashindano hayo Alphonce Felix pamoja na mkufunzi
wa timu hiyo ya Riadha Francis John wameushukuru uongozi wa Riadha kwa
kuiwezesha timu hiyo kukaa kambini kwa miezi saba na kuahidi safari hii timu
hiyo haiendi kushiriki bali kupambania medali.
Wanariadha waliopo
katika timu hiyo ya taifa wanaotarajiwa kwenda Brazili ni mwanamke pekee Sara
Ramadhani, Fabiani Joseph, Saidi Makuka na Alfonce Felix .
No comments:
Post a Comment