Pages

July 27, 2016

RAIS DKT. MAGUFULI AWAAPISHA MWENYEKITI PAMOJA NA KATIBU WA TUME YA UTUMISHI WA WALIMU (TSC) IKULU CHAMWINO MKOANI DODOMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Oliva Joseph Mhaiki kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Winfrida Gaspa Rutaindurwa kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) Oliva Joseph Mhaiki (kushoto) pamoja na Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) Winfrida Gaspa Rutaindurwa (kulia) mara baada ya kuwaapisha ) katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) Oliva Joseph Mhaiki (watatu kutoka kushoto) pamoja na Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) Winfrida Gaspa Rutaindurwa (watatu kutoka kulia) mara baada ya kuwaapisha. Wengine katika picha ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa , Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Seleman Jafo.
Rais Dkt. John Magufuli akisalimiana na Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Seleman Jafo mara baada ya tukio la uapisho katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma. Katikati ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimpongeza Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) Oliva Joseph Mhaiki mara baada ya tukio la uapisho wa Mwenyekiti huyo pamoja na Katibu wa Tume hiyo katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma. Picha na IKULU.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...