Pages

July 2, 2016

Polisi Arusha yazindua vituo vya polisi jamii

Mkuu wa Polisi wilaya ya Arusha (SSP) Emmanuel Tille akiongea na viongozi wa kata ya Moivaro tarafa ya Suye pamoja na askari wa vikundi vya ulinzi shirikishi wakati wa uzinduzi wa vikundi vinne vya kata hiyo. 

 Mkuu wa Polisi wilaya ya Arusha (SSP) Emmanuel Tille akiwakagua askari wa vikundi vya ulinzi shirikishi kutoka mitaa ya Ngurumausi, Oldonyommasi, Moivaro Kati na Shangarao. 

 Diwani wa kata ya Moivaro Rick Moiro akiongea na askari wa vikundi vya ulinzi shirikishi toka kwenye baadhi ya mitaa ya kata yake mara baada ya uzinduzi wa vikundi hivyo.

Baadhi ya viongozi wa kata ya Moivaro pamoja na askari wa vikundi vipya vya ulinzi shirikishi wakionekana kumsikiliza kwa umakini Mkuu wa Polisi wilaya ya Arusha (SSP) Emmanuel Tille hayupo pichani.

 Mmoja wa wahitimu wa askari wa ulinzi shirikishi katika kata ya Moivaro akikabidhiwa kitambulisho cha kazi kutoka kwa Mkuu wa Polisi wilaya ya Arusha (SSP) Emmanuel Tille .Picha zote na Rashid Nchimbi -Polisi Arusha

Na Magesa Magesa,Arusha
POLISI mkoani hapa imesema bila ushirikiano madhubuti kutoka kwa wananchi katika kuimarisha ulinzi Jeshi la Polisi pekee haliwezi kutimiza hazma hiyo hivyo kuwataka wananchi kuwa waangalifu  kwa kutoa taarifa zinazoashiria uvunjifu wa amani kwenye mitaa yao ili lishughulikiwe.
Aidha uanzishwaji wa  mafunzo ya polisi jamii katika mitaa ni dhana itakayosaidia kwa kiasi kikubwa udhibiti wa matukio ya kiuhalifu yanayofanywa na baadhi ya watu wachache wenye nia mbaya.
Katika hafla ya uzinduzi wa vituo vya polisi jamii katika mitaa minne iliyopo katika kata ya moivaro jijijni arusha kamanda wa polisi wilaya ya arusha Emanueli Marcko Tille alisema jeshi la polisi limeamua kuanzisha mafunzo ya polisi jamiii kwa lengo la kusaidia kupunguza matukio  madogo yanayotokea ndani ya jamii hivyo kama msimamizi mkuu atahakikisha polisi hao wanafamya kazi katika jamii bila kuwepo lawama.
Tille alisema kuwa licha ya kuwepo kwa maeneo korofi yaliyokothiri kwa matukio ya wizi na ujambazi polisi hao watakuwepo katika mitaa yao wakifanya ulinzi nyakati za usiku huku wakishirikiana na mjeshi la polisi kuhakikisha ulinzi na usalama unadumishwa sehemu ya makazi ya watuu kwani asilimia kubwa ya uhalifuu unafanywa katika mitaa.
"Matukio mengi yanayotokea yamekuwa ni miongonimwa jamii hivyo ni vyema sisis kama jeshi la polisi tuanahakikisha tunawaweka wasaidizi katika kila mitaa kufanya doria ili kuhakikish raia na mali zake wapo salama"

Diwani wa kata hiyo ya Moivaro ,Erick Moiro alisema katika kata hiyo wanachangamoto yagari la doria nyakati za usiku hvyo kupelekea kukwamisha kazi pindi wanapowakamata wahaalifu nyakati za usiku hivyo alilipomba jkeshi la polisi kufanya jitihada za dhati ili kufanikisha hilo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...