Mwenyekiti wa CCM ambaye leo anatarajiwa kukabidhi kijiti kwa Mwenyekiti Mpya,Rais wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete,akifafanua jambo wakati akisoma hotuba yake ya Mwisho katika kiti hicho.
Sehemu
ya Meza kuu kama ionekanavyo pichani tayari wamekwisha ingia ndani ya
ukumbi wa Dodoma Convetion Center (DCC) kukamilisha mchakato wao wa
kumchagua Mwenyekiti mpya wa chama hicho cha CCM.Pichani kulia ni Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana,Mwenyekiti wa CCM ambaye leo
anatarajiwa kukabidhi kijiti kwa Mwenyekiti Mpya,Rais wa awamu ya nne
Dkt Jakaya Kikwete,Makamu Mwenyekiti Zanzibar Rais Dkt Shein pamoja na
Mwenyekiiti mtarajiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John
Pombe Magufuli.PICHA NA MICHUZI JR -DODOMA.
Viongozi wakuu wa Wastaafu wa chama cha CCM na Serikali kwa ujumla wakifuatilia yanayojili ukumbini .Wajumbe wapatao zaidi ya 2000 wakifuatilia hotuba iliyokuwa ikisomwa na Mwenyekiti ambaye leo anaachia kiti hicho na kukabidhi kwa Mwenyekiti mpya Dkt John Pombe Magufuli,katika mkutano Mkuu Maalum wa CCM unaofanyika ndani ya ukumbi wa Dodoma Convetion Center (DCC),mkoani Dodoma
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitoa ratiba na miongozo
mbalimbali kwa Wajumbe wapatao zaidi ya 2000 wa mkutano Mkuu Maalum wa
CCM ambao tayari wako ndani ya ukumbi wa Dodoma Convetion Center (DCC)
kukamilisha mchakato wao wa kumchagua Mwenyekiti mpya wa chama hicho cha
CCM.
Mwanana
mahiri wa nyimbo za Taarab kutoka kundi la Tot Plus Khadija Kopa
akiimba mbele ya Wajumbe wapatao zaidi ya 2000 wa mkutano Mkuu Maalum wa
CCM ambao tayari wako ndani ya ukumbi wa Dodoma Convetion Center (DCC)
kukamilisha mchakato wao wa kumchagua Mwenyekiti mpya wa chama hicho cha
CCM.
Baadhi
ya wageni waalikwa kutoka vyama mbalimbali vya upinzani pia
wanahudhuria mkutano huu Maalum wa CCM.Ambapo vyama vya siasa vipatavyo
12 vilialikwa na vyote vimefika katika mkutano huo isipokuwa chama cha
CHADEMA.
Wajumbe
wapatao zaidi ya 2000 wa mkutano Mkuu Maalum wa CCM wakiwa tayari ndani
ya ukumbi wa Dodoma Convetion Center (DCC) kukamilisha mchakato wao wa
kumchagua Mwenyekiti mpya wa chama hicho cha CCM.
Wajumbe
wapatao zaidi ya 2000 wa mkutano Mkuu Maalum wa CCM wakitumbuizwa ndani
ya ukumbi wa Dodoma Convetion Center (DCC) ulioko nje kidogo ya mji wa
Dodoma,hivi sasa na kundi la TOT Plus likiongozwa na Mwana mama Mkongwe
Khadija Kopa,wakati huo Meza kuu ikisubiriwa kuingia ukumbini.
Baadhi
ya Wageni waalikwa wakiwemo mabalozi wa nchi mbalimbali wakiwa ndani ya
ukumbi ambapo leo mkutano Mkuu Maalum wa CCM unafanyika kwa ajili ya
kumchagua Mwenyekiti mpya wa chama cha Mapinduzi (CCM) kwa miaka
kumi,Rais John Pombe Magufuli anatarajiwa kukabidhiwa kijiti hicho
kutoka kwa Mwenyekiti ambaye anamaliza muda wake leo, Rais Mstaafu wa
awamu ya nne,Dkt Jakaya Kikwete,mkutano huo unafanyika ndani ya ukumbi
wa Dodoma Convetion Center (DCC) ulioko nje kidogo ya mji wa Dodoma.
Wajumbe
wapatao zaidi ya 2000 wa mkutano Mkuu Maalum wa CCM wakiwa tayari ndani
ya ukumbi wa Dodoma Convetion Center (DCC) kukamilisha mchakato wao wa
kumchagua Mwenyekiti mpya wa chama hicho cha CCM.
Baadhi
ya Wageni waalikwa kutoka sehemu mbalimbali wakiwa ndani ya ukumbi
ambapo leo mkutano Mkuu Maalum wa CCM unafanyika kwa ajili ya kumchagua
Mwenyekiti mpya wa chama cha Mapinduzi (CCM) kwa miaka kumi,Rais John
Pombe Magufuli anatarajiwa kukabidhiwa kijiti hicho kutoka kwa
Mwenyekiti ambaye anamaliza muda wake leo, Rais Mstaafu wa awamu ya
nne,Dkt Jakaya Kikwete,mkutano huo unafanyika ndani ya ukumbi wa Dodoma
Convetion Center (DCC) ulioko nje kidogo ya mji wa Dodoma.
No comments:
Post a Comment