Na John Nditi, Morogoro
MOTO
mkubwa umeteketeza Jengo la Idara ya Uzalishaji la Kiwanda cha 21st
Century Textiles Ltd ambapo zamani kabla ya kubinafsishwa na Serikali
kilijulikana kwa jina la Morogoro Polyester Textile Ltd ambapo bado
haikujulikana hasara iliyopatikana.
Moto
huo ulianza majira ya saa 12: 45 asubuhi ya Julai 19, mwaka huu
kwenye Kiwanda hicho kilichopo eneo Viwanda Kihonda, Manispaa ya
Morogoro.
Kufuatia
kutokea kwa moto huo, Kikosi cha Jeshi la Uokoaji na Zimamoto kwa
kushirikiana na Polisi walifika eneo la tukio mara moja na kuanza kazi
ya kuzima moto uliokuwa ukiwaka kwa nguvu juu ya paa la Jengo hilo .
Kamanda
wa mkoa wa Morogoro , Jeshi la Uokoaji na Zimamoto, Ramadhan Pilipili,
alisema licha ya kuwahi eneo la tukio, bado walikabiliana na ugumu wa
kuingia ndani hivyo kulazimika kutoboa ukuta kwa kutumia katapira ili
kupata nafasi ya uwazi ya kurusha maji ndaniya jengo ili kuuzima.
Hivyo
alisema , ndani ya jengo hilo kulikuwa na marotoba ya pamba ambayo
yalishika moto na kuwawia vigumu kuingia ndani na kulazimika kwanza
kutoboa sehemu za ukuta wa jengo ili kupenyeza maji yatakayowezesha
kuuzima moto huo.
Kamanda
wa mkoa wa Jeshi la Uokoaji na Zimamoto alisema jitihada za kuuzima
moto huo zilikuwa zinaendelea hadi majira ya saa tisa alasiri ambapo
pia waliungana na timu ya askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)
kuezesha zoezi la kuuzima moto huo.
Katika
tukio hilo, Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei
aliungana na viongozi wengine na vikosi hivyo ili kuona moto huo
unadhibitiwa ili usiweze kuleta madhara makubwa zaidi.
Kwa
upande wake Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe aliyefika
kujioenea tukio hilo alitumia fursa hiyo kuuagiza uongozi wa Jeshi la
Uokoaji na Zimamoto mkoa kufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika
viwanda.
Dk
Kebwe alisema , lengo ni kuona maeneo ya viwanda vinakuwepo vifaa vya
dharura vinavyofanya kazi ya kuzima moto unapojitokeza ikiwemo na
maeneo mengine ya majengo ya matumizi ya mkusanyiko wa kazi.
“
Maeneo kama haya ya viwanda ni lazima kuwepo na vitu vya tahadhari ,
kama sehemu za kuchota maji , vifaa vya kuzimia moto viwemo ndani ya
viwanda na maeneo mengine ili moto unapozuka iwe ni rahisi kuwahi
kuuzima” alisema Dk Kebwe.
Mbali
na hayo, pia mkuu wa mkoa alimwagiza Kamanda wa Polisi wa mkoa
kulimaisha ulinzi eneo hilo ili kuzuia vibaka na wezi kuweza kuiba mali
zilizopo.
Naye
Meneja Uzalishaji Kiwanda cha 21st Century Textiles Ltd, Clemence
Munis , alisema kuwa moto huo ulitokea kwenye Idara ya usokotaji wa
nyuzi za nguo baada ya moja ya mashine zake kutoa cheche na kurukia
katika marotoba ya pamba na kisha kuwaka moto uliokwenda kunasa kwenye
nyanya za umeme.
Munis
alisema wakati wakianza kuchukua hatua za kuzima kwa kutumia vifaa
vya kuzima ndani ya kiwanda , walikiarifu Kikosi cha Jeshi la Uokoaji
na Zimamoto pamoja na Polisi wa mko ambao walifika katika kipindi cha
muda mfupi kiwandani hapo.
“
Moto umetokea majira ya saa moja kasorobo asubuhi ya leo ( Julai 19)
sehemu ya uzalishaji baada ya kutokea hitirafu ya umeme kwenye mashine
ya kusokota pamba “ alisema Munis.
Kiwanda
hicho kina majengo na idara mbalimbali ikiwemo ya usokotaji,
useketaji na umaliziaji wa nguo na mashine zinazotukika kwa kazi hizo.
“
Nawapongeza Jeshi la Ukoaji na Zimamoto Morogoro, wamefika kwa wakati
ndani ya dakika 10 na kuanza kuzima moto wakishirikiana Polisi ,
wananchi na wafanyakazi wakiume na ninatumai zoezi litafanyikiwa kwa
haraka na mali nyingi kuokolewa” alisema Munis.
Munis
alisema hakuna madhara ya kibinadamu , isipo kuwa moto huo umetekeleza
marotoba ya pamba ,nguo na mashine zilizokuwepo katika idara hiyo
ambapo bado kiwango cha gharama halisi ya hasara iliyotokana na moto
huo kujulikana .
“
Bado hatuajua hasara kamili , isipokuwa moto huu umetekeleza mali
nyingi hasa marotoba ya pamba, nguo na mashine eneo la idara ya ufumaji
wa nguo ...na hii itajulikana baaada ya kufanyika kwa tathimini “
alisema Munis.
Kiwanda
cha 21st Century Textiles , kimuundo ni kampuni tanzu ya Mohamed
Enterprises ( TANZANIA) LTD – (MeTL) na ilianza uzalishaji mwaka 2005,
baada ya kununua katika zoezi la ubinafsishaji mali za kampuni ya umma
iliyojulikana kwa jina la MOROGORO POLYESTER TEXTILES LTD.
No comments:
Post a Comment