Pages

July 20, 2016

CHAMA CHA NCCR- MAGEUZI CHABAINI NCHI KUONGOZWA KWA MATAMKO YA RAIS BADALA YA KATIBA


Mkuu wa Idara ya Kampeni na Uchaguzi wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Faustine Sungura (kulia), akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya chama hicho, Ilala jijini Dar es Salaam leo asubuhi wakati akimkaribisha Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia (katikati), kuzungumza kuhusu maazimio yaliyofikiwa  na Kikao cha Halmshauri Kuu ya Taifa cha kawaida kilichoketi Julai 16 mwaka huu. Kushoto ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Mosena Nyambabe.
 Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu maazimio mbalimbali yaliyopendekezwa katika kikao cha Halmshauri Kuu ya Taifa ya chama hicho cha kawaida  kilichoketi Julai 16 mwaka huu. Kushoto Katibu Mkuu wa chama hicho, Mosena Nyambabe.


 wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.

Na Dotto Mwaibale

CHAMA cha NCCR Mageuzi kupitia Halmshauri yake Kuu ya Taifa kimesema kinasikitishwa na hali ya nchi hivi sasa ambayo inaongozwa kwa matamko ya Rais badala ya kufuata katiba jambo ambalo ni hatari kwa taifa.


Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa NCCR- Mageuzi Taifa, James Mbatia wakati akizungumza na wanahabari makao makuu ya chama hicho, Ilala jijini Dar es Salaam leo, kuhusu mapendekezo yaliyofikiwa na kikao hicho.

"Hivi sasa nchi inaongozwa kwa matamko mbalimbali ya Rai badala ya kufuata katiba ya nchi" alisema Mbatia.

Mbatia alisema Rais Dk.John Magufuli amekuwa akiongoza nchi kwa kutoa matamko badala ya kuongozwa kwa kufuata katiba, sheria na kanuni za nchi.

"Mfano siku akiongea na majaji aliwaamuru watoe hukumu haraka dhidi ya waliokuwa na makontena ambayo yalikuwa hayajalipiwa kodi na kuahidi kama wakilipa atawapa sehemu ya fedha hizo wakati bunge ndiyo lenye mamlaka yakuidhinisha matumizi ya pesa za serikali,"alisema Mbatia.

Alisema kutokana na tamko hilo kwa majaji ilikuwa ni kuingilia mamlaka ya Mahakama na Bunge kitu ambacho ni kinyume cha kanuni, taratibu na katiba ya nchi.

Alisema hali hiyo imesababisha demokrasia kukiukwa huku uhuru wa kujieleza (Freedom of Exptression) ukiendelea kudidimia siku hadi siku. 

Alisema kumekuwa na matumizi ya nguvu za dola kupitia jeshi la polisi kwa kuzuia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa kwa kuwakamata na kuwaweka rumande viongozi wa kisiasa na kuwashtaki kwa  makosa mbali mbali.

"Viongozi wakisiasa wamekuwa wakikamatwa na Jeshi la Polisi kwa makosa mbali mbali lakini kinachofanyika ni ukiukwaji wa uhuru na hazi za vyama vya siasa katika kufanya kazi zao ambazo zipo kikatiba pamoja na sheria za vyama vya siasa,"alisema.

Kwa upande mwingine chama hicho kupitia maazimio ya kikao cha Halmashauri Kuu ya chama kimetangaza kumsimamisha uongozi wa Umakamu Mwenyekiti (Bara) na kumvua uanachama Leticia Ghate Mosore kwa makosa mbali mbali aliyoyafanya ndani ya chama.

Mbatia alisema wameamua kumsimamisha uongozi na kumvua uanachama kwa kukiuka kanuni na katiba ya chama hicho ikiwa ni pamoja na usaliti alioufanya kipindi cha uchaguzi mkuu wa mwaka jana.

"Kwa jumla makosa aliyoyafanya ni pamoja kujihusisha na migogoro ndani ya chama, kutoa tuhuma dhidi ya kiongozi wa cham au mwanachama nje ya utaratibu, kukashifu kiongozi wa chama au mwanachama, kuhujumu chama katika uchaguzi na wakati mwingine wowote na kutoa na kupokea rushwa," alisema Mbatia.

Alisema milango iko wazi kwa Leticia kukata rufaa kama atakuwa hajaridhika na maamuzi hayo na rufaa yake itasikilizwa na kama ataonekana hana hatia juu ya makosa hayo atarudisha kundini.

Aidha kuhusu chama chake kushiriki katika muungano wa Umojka wa kaiba ya wananchi (Ukawa), alisema chama hicho kitaendelea kushirikiana na vyama hivyo kwa nguvu zote.

Alisema kupitia umoja huo chama chake kipo pamoja na wanachi katika kupambana na kupigania kuhakikisha katiba mpya inapatikana kama matakwa yao wananchi wenyewe.

Alisema ikiwa Jaji Lubuva ataleta katiba ile iliyopitishwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) watapiga kampeni za kuipinga kwa nguvu zote mpaka itakapopatikana katiba inayokidhi mahitaji ya wananchi.




No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...