Pages

June 19, 2016

WATOTO WENYE AKAUNTI ZA JUNIOR JUMBO WAZAWADIWA ZAWADI NA BENKI YA CRDB TAWI LA WATER FRONT JIJINI DAR ES SALAAM

WATOTO WENYE AKAUNTI ZA JUNIOR JUMBO WAZAWADIWA ZAWADI NA BENKI YA CRDB TAWI LA WATER FRONT JIJINI DAR ES SALAAM .

KATIKA kusherekea siku ya mtoto wa Africa, Bank ya CRDB Tawi la Water Front  limetoa zawadi mbali mbali kwa watoto wenye akaunti ya Junior Jumbo pamoja na kula  keki pamoja na kunywa vinywaji nao, Katika kusherekea siku hii adhimu na muhimu.

Akitoa shukrani kwa niaba ya wazazi wengine waliowafungulia akaunti katika benki hiyo amewanashkuru sana kwa  kuwapa zawadi watoto wao na iwe chachu kwa wazazi wengine kuafungulia akaunti watoto wao.

Keki na zawadi kwaajili ya watoto wenye akaunti ya Junior Jumbo katika Benki ya CRDB tawi la Water Front.
Meneja Biashara wa Benki ya CRDB tawi la Water Front jijini Dar es Salaam, Adam Akaro akimkaribisha Meneja wa Tawi hilo  kwaajili ya kuwakaribisha wazazi pamoja na watoto wao walifika katika tawi la Water Front jijini Dar es Salaam leo.
Meneja wa benki ya CRDB tawi la Water Front, Timoth Shirima akizungumza na wazazi pamoja na watoto wenye akaunti katika tawi hilo kwaajili ya kufurahi pamoja na watoto wenye akaunti za benki za Junior Jumbo katika tawi hilo. Shirima pia ameuliza maswali watoto hao na watoto wanaojibu vizuri amewapa zawadi.

 Watoto wakinyoosha  mkono kujibu maswali ya Meneja wa Tawi la Water Front, Donath Sheirima jijini Dar es Salaam leo. Pia waliojibu maswali vizuri wamepewa zawadi mbalimbali ambazo zilikuwa zimeandaliwa kwaajili ya watoto hao katika tawi hilo.
 Watoto wakiwasha mishumaa.
  Zawadi.
Watoto wakiwa kwenye foleni kwenda kuweka Fedha kwenye akaunti zao za Junior Jumbo katika tawi la Water Front jijini Dar es Salaam leo. 
 Wazazi wakipiga picha zawadi za watoto.
  

  Watoto wakisikiliza kwa makini maswali yanayoulizwa na Meneja wa Tawi la Water Front, Donath Shirima jijini Dar es Salaam leo.
Meneja Rasilimali watu wa Benki ya CRDB makao makuu, Timoth Fasha akikata keki kwaajili ya watoto wenye akaunti ya Junior Jumbo katika Tawi la Water Front jijini Dar es Salaam.
Watoto na wazazi wakifurahia Shampein ilivyofunguliwa jijini Dar es Salaam.
 Meneja Rasilimali watu wa Benki ya CRDB makao makuu, Timoth Fasha akiwalisha keki wazazi na watoto wenye akaunti ya Junior Jumbo katika tawi la Water Front jijini Dar es Salaam . 
Meneja huduma kwa wateja Tawi la Water Front, Mary ngowi akiwa na mtoto mwenye akaunti ya Junior Jumbo Zainul Ally katika tawi hilo.


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...