UEFA
imezitahadharisha England na Russia huenda zikaondolewa kwenye michuano
ya Euro 2016 kama vurugu zao zilizotokea kwenye mchezo wao wa ufunguzi
huko Marseille zitaendelea.
Matukio
tofauti kabla na wakati wa mchezo huo wa Jumamosi wa Kundi B yanaonesha
idadi kubwa ya mashabiki wamejeruhiwa huku shabiki mmoja wa England hali
yake ikiwa mbaya hospitali.
Kwenye
kauli yao, Kamati ya Utendaji ya UEFA imesema: “Hatutasita kuweka
vikwazo kwa vyama vya soka Football Association (FA) na Russian Football
Union (RFU) ikiwa ni pamoja na kuziondoa timu kwenye mashindano kama
vurugu hizo zitatokea kwa mara nyingine.
Warussia
wametuhumiwa kusababisha usumbufu, matukio ya kibaguzi pamoja na
kuharibu miundombinu ya mbalimbali uwanjani wakati England wao wamepewa
karipio kali kwa maandishi.
FA pia
wameambiwa kuwataarifu mashabiki wanaosafiri kutoka England kwenda
Ufaransa kuishangilia timu yao, kujali wajibu wao unaowapeleka huko hasa
katika kipindi hiki cha majira ya joto.Taarifa ya UEFA inasomeka:
“Kamati ya Utendaji ya UEFA inapenda kusema kwamba, imesikitishwa na
vitendo vya vurugu vilivyotokea kwenye jiji la Marseille.”
“Vitendo
hivyo visivyokubalika kutoka kwa wanaojiita mashabiki wa timu za taifa
za England na Russia havina nafasi kwenye mchezo wa soka, mchezo ambao
ni lazima tuulinde na tuutunze.”
“Kamati
tendaji ya UEFA imevionya vyama vya soka vya nchi zote kwamba, maamuzi
yoyote yatakayotolewa na na kamati huru ya nidhamu kuhusiana na matukio
ya ndani ya uwanja, hatutasita kutoa adhabu ya ziada ikiwa ni pamoja na
kuvifungia vyama vya soka Football Association (FA) na Russian Football
Union (RFU) pamoja na kuziondoa timu zao kwenye mashindano kama vurugu
hizo zitajitokeza mara nyingine.”
“Tunavitaka
vyama vyote vya soka FA pamoja na RFU kuwataka mashabiki wao
kushangilia timu zao kwa nidhamu na utaratibu unaokubalika.”
“Pia
tunavishukuru vyombo vya ulinzi na usalama vya Ufaransa kwa nguvu zao
kutuliza na kuyaokoa mashindano kutoka wenye changamoto hiyo.”
Hatua za
kinidhamu zinaendelea kufutia vurugu zilizotokea kwenye mchezo wa UEFA
EURO 2016 hatua ya makundi kati ya England na Russia uliomalizika kwa
sare ya kufungana bao 1-1
Mashtaka yanayokikabili chama cha soka cha Russia (Football Union of Russia) ni pamoja na:
Vurugu na kusababisha usumbufu kwa kundi la watu
Tabia za kibaguzi
Kuharibu miundombinu
Kesi hii itasimamiwa na UEFA chini ya bodi ya nidhamu na maadili kuanzia June 14
No comments:
Post a Comment