Katika
kuendelea kuimarisha ushirikiano uliopo kati ya walipa kodi na
wakusanyaji wa kodi, Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) imefanya kongamano
la pamoja na wadau wa kodi nchini likiwa na lengo la kujadili kwa pamoja
kuhusu uanzishwaji wa chombo cha kuratibu na kusimamia wanataaluma wa
kodi.
Akizungumza
wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo, Kamishna wa Sera na Bajeti kutoka
Wizara ya Fedha na Mipango, Shogholo Msangi alisema wamekutanisha wadau
hao wa kodi ili waweze kutoa maoni na kukubaliana kwa pamoja jinsi gani
chombo hicho kitaweza kufanya kazi.
"Kutakuwa
na chombo ambacho kitakuwa kinaratibu na kusimamia wanataaluma wa kodi
na lengo ni kupitia kongamano hilo wadau wa kodi wataweza kukubaliana
kwa pamoja kuona ni jinsi gani chombo hicho kitafanya kazi,
Kamishna
wa Sera na Bajeti kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Shogholo Msangi
akitoa neno la ufunguzi katika kongamano lililoandaliwa na TRA na
kukutanisha wadau mbalimbali wa kodi. (Picha zote na Rabi Hume - MO
Blog)
"Unaweza
kukuta kuwa mlipa kodi kwa sasa ndiyo anaumia au TRA ndiyo inaumia
lakini chombo hicho kitaweza kusimamia na kuweka kila jambo sehemu
sahihi kama linavyotakiwa kuwapo," alisema Msangi.
Nae
Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Kodi (ITA), Prof. Isaya Jairo alisema kuwa
chombo hicho kama kikianzishwa kitaweza kufanya kazi zake kwa uhuru bila
kuingiliwa na TRA ili kuhakikisha kuwa kinatoa na haki kati ya mlipa
kodi na wakusanyaji wa kodi (TRA) bila kuumiza upande wowote kwani jambo
hilo linawahusu wote.
Mkuu
wa Chuo cha Taifa cha Kodi (ITA), Prof. Isaya Jairo akitoa neno la
ukaribisho katika ufunguzi wa kongamano hilo lililofanyika Bagamoyo,
Pwani.
Alisema
kupitia kongamano hilo wamekutanisha wataalam wa kodi, wahasibu, walipa
kodi, wanasheria, washauri wa kodi na walimu wa kodi kutoka vyuoni ili
kuweza kupata maoni ya pamoja na kupata maoni ya makubaliano ya pande
zote ambayo yatatumika katika kuendesha chombo hicho.
Na Rabi Hume - MO Blog)
Baadhi ya wadau waliohudhuria kongamano hilo la siku moja lililofanyika Bagamoyo, Pwani.
Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja (group one).
Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja.
No comments:
Post a Comment