SERIKALI
kupitia Bodi ya Utalii Nchini (TTB) na Shirika la Hifadhi za Taifa
Tanzania (TANAPA), katika mwaka 2016/17 imetenga kiasi cha Tsh. Bilioni
2.7 kwa ajili ya kuitangaza sekta ya utalii ndani na nje ya nchi.
Akijibu
swali la mbunge wa Viti Maalum (CCM), Maria Kangoye, leo Bungeni Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani alisema bajeti hiyo
ni ongezeko la asilimia 14.7 za fedha za Serikali zilizotengwa katika
bajeti ya mwaka ya 2015/16.Makani
alisema Serikali itaendelea kuboresha sekta ya utalii kwa kushirikisha
wadau mbalimbali wa maendeleo na vyanzo vingine vya mapato kama
ilivyoanishwa katika mpango wa maendeleo wa miaka mitano 2016/17-
2020/21.
Alisema
Serikali pia imepanga kuimarisha Chuo cha Utalii katika kampasi za
Bustani iliyopo Dar es Salaam, Temeke na Arusha ikiwa ni pamoja na
kuongeza idadi na umahiri wa wakufunzi, kuboresha upatikanaji wa vifaa
vya kufindishia na kuboresha miundombinu ya kampasi hizo.
“Kuhusu
uimarishaji wa miundombinu, Wizara yangu imetenga jumla ya Tsh. Milioni
500 katika bajeti ya mwaka 2016/17 ili kukamilisha ujenzi wa jengo la
Utalii katika Bustani ya Chuo cha Utalii Tanzania” alisema Mhandisi
Makani
Aidha
Mhandisi Makani alisema kuwa Chuo cha Utalii Tanzania kwa kushrikiana
na Chuo cha Vancouver University cha Canada kupitia mradi wa ISTEP
uliopo chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ya Ufundi
kitaanzisha mafunzo ya Uongozi katika shahada kuanzia mwezi septemba
2018.
Aidha
Mhandisi Makani alisema Serikali inaendelea kuelekeza nguvu katika vyuo
vilivyopo kwa kuongeza idadi ya wahitimu wa ngazi ya kati na baadaye wa
ngazi ya shahada, ambapo kwa sasa Chuo cha Utalii Tanzania kitaanza
kuboresha utoaji wa mafunzo katika tansia za ukarimu na Utalii katika
ngazi ya shahada.
No comments:
Post a Comment