Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
jambo wakati akiagana na Mchungaji Anthony Lusekelo‘Mzee wa Upako’
katika kanisa lake la Maombezi lililopo Ubungo Kibangu jijini Dar es
Salaam. Rais Dkt. Magufuli alihudhuria ibada hiyo pamoja na kukagua
barabarainayotoka Ubungo Kibangu hadi Barabara ya Mandela eneo la
Riverside.
Mchungaji
wa Kanisa la Maombezi Mchungaji Anthony Lusekelo‘mzee wa upako akiagana
na mke wa Rais Mama Janeth Magufuli mara baada yakuhudhuria ibada
katika Kanisa la Maombezi Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam. Kushoto
ni Rais Dkt. Magufuli akiwashukuru waumini wa kanisa hilo.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe
Mama Janeth Magufuli wakati wakitoka kwenye kanisa
la Maombezi la Mchungaji Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’ Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam. (PICHA NA IKULU)
No comments:
Post a Comment