Ole Medeye akionesha kati ya uanachama ya UDP
Aliyekuwa mfuasi wa Chadema Goodlack Ole Madeye leo amehamia Chama cha UDP kwa kile alichodai ndani ya chama hicho hakuna demokrasia ya kweli.
Amesema anachukizwa na kitendo cha wabunge wa chama hicho na vyama vingine vya upinzani kususia vikao vya Bunge.
Ole Madeye ambaye amehamia chama hicho ikiwa ni baada ya miezi tisa tangu alivyojiunga na Chadema akitokea CCM Agosti 2015, amekabidhiwa kadi ya UDP na Mwenyekiti wa chama hicho, John Cheyo akiwa na wafuasi wengine tisa wapya kutoka Chadema akiwamo mke wake, Anatonia Lekule.
Amesema alipitia katiba za vyama vyote hajaona katiba inayosimamia misingi ya kidemokrasia ya kweli na kwamba UDP ndiyo chama pekee Tanzania chenye katiba inayotetea demokrasia.MWANANCHI

No comments:
Post a Comment