Pages

June 1, 2016

Naibu Waziri Masauni kafika msitu wa mapangopori ya Amboni yanayodaiwa kuwa njia ya majambazi

Taarifa iliyochukua vichwa vya habari vya magazeti ya leo June 01 2016 ni kuhusu mauaji ya watu wanane waliouawa na watu wanaodhaniwa ni majambazi katika kata ya Mzizima, tarafa ya Chumbageni jijini Tanga.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ametembelea eneo hilo la msitu wa mapangopori ya Amboni na baadaye kuzungumza na wakuu wa vyombo vya ulinzi.
Msitu wa Mapangopori ya Amboni ndio unaodaiwa kuwa ni njia kuu ya watu wanaohofiwa ni majambazi waliofanya mauaji katika Kitongoji cha Kibatini, Kata ya Mzizima, Tarafa ya Chumbageni, Tanga.
PIX 2
Mhandisi Hamad Masauni, Kamanda wa Polisi Tanga, Leonard Paulo (kulia) na Mkuu wa Kikosi Maalum kutoka Kikosi cha Kutuliza Ghasia Makao Makuu Dar es Salaam, Mratibu Mwandamizi wa Polisi, William Mwampagale (katikati).
PIX 3
.
PIX 4
Mhandisi Hamad Masauni na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigella
PIX 1

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...