Tukio
hilo limefanyika leo kuanzia katika Ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga na
kuhudhuriwa na waumini na viongozi wa dini ya mbalimbali wakiongozwa
na Sheikh Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ismail Habibu Makusanya.
Wengine
waliohudhuria ni viongozi wa vyama vya siasa na serikali,viongozi wa
madhehebu mengine ya dini wakiongozwa na Askofu wa Kanisa la Africa
Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga, Askofu Dr. John
Nkola na watu mbalimbali wenye mapenzi mema.
Akizungumza
wakati wa kula chakula cha pamoja “Futari” mwandaaji wa chakula hicho
ambaye ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Erasto Kwilasa alisema
aliwashukuru waumini wa dini ya kiislamu kukubali kushiriki na kudai
kuwa ameamua kufanya hivyo ili kuonesha kwa vitendo kuwa anawapenda watu
wa Shinyanga bila kujali makabila,dini wala rangi zao.
“Nawashukuruni
sana tumekusanyika hapa,tupo hapa katika kushirikiana pamoja kwa kupata
futari ya pamoja,mimi binafsi naamini katika ibada hii tutakuwa
tumetenda jambo jema mbele ya mwenyezi mungu hasa katika kutekeleza
nguzo muhimu miongoni mwa nguzo tano za kiislamu,funga ya mwezi
mtukufu”,alisema Kwilasa.
“Ndugu
zangu mlikuwa na nfasi ya kutoa udhuru kwamba mimi ni kiongozi wa
chama,lakini kwa upendo mlionionesha leo hii,mmedhihirisha ule usemi wa
serikali na chama havina dini bali wanachama wake wana dini zao na hii
ndiyo maana mmekuja kwa wingi na mpaka sasa tupo pamoja hapa bila
ubaguzi wa aina yoyote”,aliongeza Kwilasa.
Kwilasa
alitumia fursa hiyo kuwataka wanasiasa kuacha kubaguana kwani binadamu
wote ni wa mwenyezi mungu huku akimuomba mungu kupokea funga za waumini
wote wa mkoa wa Shinyanga na taifa kwa ujumla.
“Kwa
kutambua kazi nzuri zinazofanywa na rais John Pombe Magufuli na timu
yake yote,naomba tuendelee kumuombea sana kwa mungu ili aweze
kufanikisha malengo yake aliyowaahidi wananchi”,alisema Kwilasa.
Katika
hatua nyingine Kwilasa aliwaomba viongozi wote wa madhehebu ya dini
kusaidiana na viongozi wa serikali mkoa wa Shinyanga kupiga vita vitendo
vya mauaji dhidi ya vikongwe,ubakaji na ulawiti kwa watoto,utumiaji wa
madawa ya kulevya na ukatili wa kijinsia.
Kwa
upande wake Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sheikh Ismail Habibu
Makusanya alimpongeza mwenyekiti huyo wa CCM kuandaa chakula cha pamoja
kwa ajili ya waumini wa dini ya kiislamu na kusema kuwa kitendo
alichokifanya kina dhawabu kubwa kwa mwenyezi mungu.
“Ukimuona
mja anashughulika kuwalisha watu, wa kweli na wasio wakweli,wacha mungu
na wasio wacha mungu huyu ameshika kazi ya mungu..sasa mwenyeji wetu
ulichokifanya hapa sisi hatuwezi kukulipa lakini hiki ulichofanya ni
kafara kubwa sana katika maisha yako ,ni hifadhi kubwa sana katika
maisha yako,ni sadaka kubwa sana,kuwaita na kuwalisha waliofunga ni kazi
kubwa,mungu akuzidishie pale ulipotoa”,aliongeza Sheikh Makusanya.
Naye
Askofu wa Kanisa la Africa Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya
Shinyanga, Askofu Dr. John Nkola alisema ni mara kwanza yake ya kwanza
kukaribishwa kwenye futari kubwa kama hiyo na kuwashukuru waislamu
kukusanyika pamoja kushiriki pamoja kwa futari na kwamba mfungo wa mwezi
mtukufu wa Ramadhani ni kwa ajili ya utukufu wa mungu.
Askofu
Nkola alitumia fursa hiyo kuwataka watanzania kujenga mshikamano na
umoja uliopo kwani umoja wa madhehebu ya dini ndiyo uzima na amani ya
taifa la Tanzania.
“Tukishikamana
na kumhubiri mwenyezi mungu ambaye ni wa amani,nchi yetu itaendelea
kuwa na amani sana,tuendelee kushikamana,na tuendelee kumuombea rais
Magufuli anafanya mambo makubwa ambayo siyo kila mtanzania atayapenda
hata kidogo”,alisema Askofu Nkola
“Sasa
sisi kazi yetu siyo siasa lakini maandiko na misahafu inatuagiza
kuwaombea wale ambao mwenyezi mungu amewapa madaraka ya
kutawala,tumuombee sana rais wetu,pamoja na serikali yetu na nchi yote
kwa ujumla tuendelee kutulia kwa amani,tuendelee kuwa kimbilio la
wanyonge wanaonyanyaswa katika nchi zao”,aliongeza askofu Nkola.
Malunde1
blog huwa haipitwi na matukio,Mwandishi mkuu wa mtandao huu,Kadama
Malunde alikuwepo eneo la tukio,ametusogezea picha 85..Shuhudia mwenyewe
hapa chini
Juni
29,2016 kumefanyika tukio muhimu mjini Shinyanga ambapo Mwenyekiti wa
Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga ndugu Erasto Kwilasa (pichani)
amewaandalia chakula cha pamoja “futari” waumini wa dini ya kiislamu
mkoa wa Shinyanga ikiwa ni sehemu ya kuutukuza mwezi mtukufu wa
Ramadhani.
Wa
kwanza kushoto ni Askofu wa Kanisa la Africa Inland Church Tanzania
(AICT) Dayosisi ya Shinyanga, Askofu Dr. John Nkola,wa kwanza kulia ni
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sheikh Ismail Habibu Makusanya wakiwa
katika ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga usiku huu
Wa
pili kutoka kushoto ni mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga Gulah
Hafeez Mukadam akiwa na viongozi wa dini ya kiislam mkoa wa Shinyanga
Mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Shinyanga ambaye ndiye mwandaaji wa Futari hiyo ndugu
Erasto Kwilasa akizungumza ukumbini na kuwashukuru waumini wa dini ya
kiislamu kwa kujitokeza kwa wingi kufuturu kwa pamoja
Mwenyekiti
huyo wa CCM mkoa wa Shinyanga ndugu Erasto Kwilasa alisema
wamekusanyika hapo kwa ajili ya kuutukuza mwezi mtukufu wa Ramadhani
Tunamsikiliza Kwilasa..... |
Kwilasa
alisema ameandaa futari hiyo ikiwa ni ishara ya kuonesha ushirikiano
kwa vitendo ikiwa ni mambo aliyousiwa na wazee wa mji wa Shinyanga
alipokutana nao na kufanya mazungumzo kwamba miongoni mwa usia wao
mkubwa ni kujitahidi kuwa karibu na watu.
Meza kuu wakitafakari...
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga akitoa hotuba fupi
Tunafuatilia hotuba.....
No comments:
Post a Comment