Mkufunzi
wa maswala ya biashara Mama Rehema Kasule kutoka nchini Uganda
akiwapa elimu wanafunzi wa Manjano Foundation jinsi ya kukabiliana na
changamoto zinazowakabili kwenye majukumu yao ya kila siku ikiwemo
kutengeneza uhusiano na watu waliofanikiwa kwa kuwa itasaidia kujifunza
mengi.Pia
namna ya kujiamini kuwaza mafanikio zaidi kuwa lazima wafanikiwe na
kuachana kabisa na mawazo ya kushindwa akiwa sambamba na Afisa mtendaji
mkuu wa Shear illusions, Mama Shekha Nasser.
Akieleza
zaidi Mama Kasule amewataka Washiriki wa Manjano Dream Makers kama
wanataka kufanikiwa kazi zao za upambaji na biashara zao ni lazima
wafanye kwa moyo mmoja kutoka ndani ya nafsi pia kuachana na fikra za
kukata tamaa na maneno ya watu ya kuwakatisha tamaa. Kwa upande afisa
mtendaji mkuu wa Shear illusions na Mkurugenzi wa Manjano Foundation
mama Shekha Nasser amewataka washiriki hao kuongeza juhudi pia
kuyatekeleza kwa vitendo yale yote waliofundishwa katika mafunzo hayo.
Mama
Rehmah Kasule alikuwa jijini Dar akihudhuria kwenye semina ya siku 4 ya
#PSIPSE "Partnership to Strengthen Innovation and Practices in
Secondary Education.
Baada
ya semina yake, mama Kasule akajitolea siku moja kuja kutoa mafunzo kwa
washiriki wa Manjano Dream Makers ikiwa ni mojawapo ya mkakati wa
washiriki walio wengi wa Vital Voices (na yeye akiwa mmojawapo) kwamba
kila mwanamke ajitolee kuwasaidia au kuwafundisha wanawake vijana kitu
anachokijua, yaani "Pay it Forward."
No comments:
Post a Comment