Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Irene
Isaka akitoa hotuba ya ufunguzi wa semina ya siku tano kwa madaktari
wanaotoka mikoa ya kanda ya ziwa kuhusu ajali na magonjwa yanayotokana
na kazi Jijini Mwanza. Bi. Isaka alisisitiza umuhimu wa WCF na madaktari
kufanya kazi pamoja ili waweze kulipa fidia stahiki kwa wafanyakazi
wote kutoka sekta Binafsi na Umma. Wengine pichani kutoka kushoto ni
Afisa Utumishi Mkuu, Mkoa wa Mwanza, Bw. Salvatory KyaKyarwenda,
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba na Mwenyekiti wa Bodi ya
Wadhamini wa Mfuko huo, Bw. Emmanuel Humba.
NA K-VIS MEDIA, MWANZA
MKURUGENZI
Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) Bi
Irene Isaka ameipongeza Bodi ya Wadhamini na Mkuurgenzi Mkuu wa Mfuko wa
Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), kwa kuweza kuwafikia wadau wake muhimu
kwanza kabla ya kuanza kutoa Fidia kwa Wafanyakazi.
Bi
Isaka aliyasema hayo leo Juni 6, 2016 wakati akifungua mafunzo ya siku
tano kwa madaktari 124 kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa kwenye ukumbi wa
jengo la PPF Plaza jijini Mwanza.Aidha, amesema kuwa sasa hivi
wafanyakazi wasifanye kazi kwa wasiwasi kwani kuna chombo maalumu
ambacho ndiyo kinga na msaada wao endapo watapatwa na majanga katika
utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Pia
Bi. Isaka ametoa wito kwa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), na
madaktari kote nchini kufanya kazi pamoja ili waweze kulipa fidia
stahiki kwa wafanyakazi wote kutoka sekta Binafsi na Umma.
Mfuko
wa Fidia Kwa Wafanyakazi, ni taasisi ya Serikali iliyoko Ofisi ya Waziri
Mkuu, na ulianzishwa kwa sheria ya Fidia Kwa Wafanyakazi namba 20 ya
mwaka 2008. Lengo la kuanzishwa kwake ni kuhakikisha Mfanyakazi anapata
fidia stahiki kutokana na kuumia kazini au magonjwa yatokanayo na kazi
na kwa wanafamilia kupokea fidia kwa niaba ya mwenza wao aliyefariki
akiwa kazini.
Mafao
yatolewayo na Mfuko huo ambayo kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa WCF,
Masha Mshomba ni pamoja na Fao la matibabu, fidia ya ulemavu wa muda,
fidia ya ulemavu wa kudumu, Fidia ya huduma ya marekebisho
(Rehabilitation services), Fedha za uangalizi wa mara zote, (Constant
attendance care grant), Fedha za mazishi, na fidia kwa wategemezi wa
mfanyakazi aliyefariki akiwa kazini au kutokana na maradhi
yaliyosababishwa na kazi aliyokuwa akifanya. “Mfuko utaanza kutoa mafao
ya kwanza kabisa tangu uanzishwe kuanzia mwaka wa fedha unaoanza Julai,
2016/2017.” Alisema Mkurugenzi Mkuu, Bw. Masha Mshomba.Mafunzo hayo
yanatolewa kwa ushirikiano wa WCF na Shirika la Kazi Duniani, ILO.
Mwenyeketi wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Emmanuel Humba akitoa hotuba yake.
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, akizungumza mwanzoni mwa mafunzo hayo.
Baadhi ya Madaktari, wakufunzi kutoka ILO wakifuatilia maelezo ya utangulizi
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo
Mkurugenzi Mkuu, Bw. Masha Mshomba, akifafanua baadhi ya mambo kwa waandishi wa habari
Picha ya pamoja
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii, (SSRA), Irene Isaka
(kulia), akisalimiana na mtaalamu wa ajali na magonjwa yanayosababishwa
na kazi kutoka Shirika la Kazi Duniani, (ILO), Dkt. Jacque Palletier
No comments:
Post a Comment