Manchester
United wamekamilisha usajili wa beki wa kimataifa wa Ivory Coast, Eric
Bailly kutoka Villareal.Beki huyo mwenye umri wa miaka 22 amejiunga na
United kwa ada ya uhamisho isiyopungua paundi millioni 30 na kusaini
mkataba wa miaka 4.
Wakati
akitambulishwa kwa waandishi wa habari Bailly alisema: “Ni ndoto
iliyokamilika kujiunga na Manchester United. Kucheza soka katika ngazi
ya juu zaidi ndio jambo ambalo nimekuwa nataka siku zote.”Manager wa Man
United Jose Mourinho alisema: “Eric ana uwezo wa kuwa mmoja wa
wachezaji bora ulimwenguni.”
Alijiunga
na Villarreal kwa £4.4m mnamo January 2015 na kucheza kila mechi huku
akiisadia timu yake ya Taifa kushinda ubingwa wa AFCON wiki kadhaa
mbele.
Bailly ni mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Mourinho tangu mreno huyo alipoqnza kazi Old Trafford.
Bailly anakuwa beki ghali zaidi katika historia ya Manchester United tangu ulipofanyika usajili wa Rio Ferdinand.
No comments:
Post a Comment