Baada
ya kufanyika nchini kwa miaka 10, mradi wa SCMS ambao ulikuwa
ukisimamiwa na John Snow Incorporated (JSI) kwa ushirikiano na Wizara ya
Afya, Ustawi wa Jamii Jinsia, Wazee na Watoto, Shirika la Misaada la
Watu wa Marekani (USAID) limeiahidi serikali ya Tanzania kuwa
litaendelea kuisaidia katika misaada mbalimbali ya afya licha ya
kumalizika kwa mradi huo.
Hayo
yamesemwa na Naibu Mkurugenzi wa USAID nchini, Tim Donnay katika
mkutano ambao ulikutanisha wadau mbalimbali wa afya ili kujadili mradi
wa SCMS ambao umefikia tamati baada ya kufanyika nchini kwa miaka 10.
Bi.
Donnay alisema serikali ya Marekani kupitia USAID imejipanga kuendelea
kuisaidia Tanzania katika sehemu mbalimbali ambazo zinahusu Afya.
“USAID
itaendelea kuisaidia Tanzania ili kuwezesha kufikiwa kwa malengo ya
upatikanaji wa huduma bora wa kiafya ... kumalizika kwa mradi huu
hukutafanya kusitishwa kwa huduma ambazo zinatolewa kwa sasa,” alisema
Bi. Donnay.
Naibu
Mkurugenzi wa USAID nchini, Tim Donnay akiwasilisha ujumbe kwa niaba ya
serikali ya Marekani katika mkutano wa hitimisho wa mradi wa SCMS.
Nae
mgeni rasmi katika mkutano huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Ustawi
wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dr. Mpoki Ulisubya alisema kufanyika
kwa mradi huo nchini kumewezesha kusaidia kuboreshwa kwa kasi huduma za
afya tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.
“Mradi
huu umetusaidia sana awali hata utolewaji wa dawa kwa waathirika wa
UKIMWI ulikuwa ni laki na nusu kwa mwaka ila kwa sasa kuna upatikanaji
wa dawa hadi laki nane kwa mwaka,
“Mbali
na hiyo pia wametujengea maghala ambayo yanatumika kuhifadhi dawa na
hata kusaidia kuweza kuwasogezea huduma wananchi ambazo awali hazikuwa
zikitolewa,” alisema Ulibusya.
Na Rabi Hume, MO Dewji Blog
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dr.
Mpoki Ulisubya akitoa neno la shukrani kwa niaba ya serikali katika
mkutano wa hitimisho la mradi wa SCMS uliotolewa na USAID na kusimamiwa
utekelezaji wake na John Snow Incorporated (JSI) kwa kushirikiana na
Wizara ya Afya. (Picha zote na Rabi Hume, MO DewjiBlog)
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar, Dr. Juma Malik Akil akitoa neno la
shukrani kwani niaba ya serikali ya Zanzibar baada ya kumalizika kwa
mradi wa SCMS.
Mfamasia
wa Serikali, Henry Irunde akielezea utaratibu wa usambazaji wa dawa
nchini uliotumika wakati ambao mradi huo ulikuwa ukifanyika nchini.
Baadhi ya wadau wa sekta ya afya walioshiriki mkutano huo.
Mkurugenzi wa John Snow Incorporated (JSI), Deo Kimera akizungumzia Mradi wa SCMS.
Baadhi
ya wafaidika wa mradi wa SCMS wakielezea jinsi mradi huo umeweza
kuwasaidia wao binafasi na katika sehemu ambazo wanafanyia kazi.
Baadhi
ya wahudhuriaji wa mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa
wa Mwalimu Nyerere wakiwasikiliza wafaidika wa mradi wa SCMS.
Muonekano wa kazi ambazo zimefanywa na mradi wa SCMS kwa kipindi cha miaka 10 tangu ulipoanza mwaka 2005.
No comments:
Post a Comment