Pages

May 28, 2016

IDADI YA VIFO KWA WATOTO WACHANGA NA WAKINA MAMA VYAZIDI KUPUNGUA NCHINI.

Balozi wa Ujerumani Mhe. Egon Kochanke kulia akikata utepe kuashilia kuanza rasmi kwa maonesho ya picha yanayofanyika Makumbusho ya Taifa mpaka Juni 10 mwaka huu jijini Dar es salaam na wa kwanza kushoto ni Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Afya , maendeleo ya Jamii , Jinsia na Watoto , Mkurugenzi wa Tiba Dkt. Margaret Mbando.
Balozi wa Ujerumani Mhe. Egon Kochanke akiongea na waandishi wa habari na Wadau wa Mpango wa Tanzania na Ujerumani kusaidia Afya (TGPSH) hawapo pichani wakati wa ufunguzi wa maonesho ya picha yanayofanyika Makumbusho ya Taifa mpaka Juni 10 mwaka huu jijini Dar es salaam.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Afya , maendeleo ya Jamii , Jinsia na Watoto , Mkurugenzi wa Tiba Dkt. Margaret Mbando akiongea na waandishi wa habari na Wadau wa Mpango wa Tanzania na Ujerumani kusaidia Afya (TGPSH) hawapo pichani wakati wa ufunguzi wa maonesho ya picha yanayofanyika Makumbusho ya Taifa mpaka Juni 10 mwaka huu jijini Dar es salaam.
Mshauri wa ufundi kutoka Mpango wa Tanzania na Ujerumani kusaidia Afya (TGPSH) Dkt. Baltazar Ngoli wa kwanza kulia akitoa maelekezo ya picha kwa Balozi wa Ujerumani Mhe. Egon Kochanke wa pili kulia pamoja na Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Afya , maendeleo ya Jamii , Jinsia na Watoto , Mkurugenzi wa Tiba Dkt. Margaret Mbando wa tatu kulia wakati wa ufunguzi wa maonesho ya picha yanayofanyika Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam.
Wadau mbalimbali wa Mpango wa Tanzania na Ujerumani kusaidia Afya (TGPSH) wakifuatilia kwa makini maelezo ya Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Afya , maendeleo ya Jamii , Jinsia na Watoto , Mkurugenzi wa Tiba Dkt. Margaret Mbando hayupo pichani wakati wa ufunguzi wa maonesho ya picha yanayofanyika Makumbusho ya Taifa mpaka Juni 10 mwaka huu jijini Dar es salaam.Picha zote na Ally Daud-Maelezo


Na Ally Daud- maelezo

Idadi ya vifo kwa watoto wachanga na wakina mama vinazidi kupungua kutoka siku hadi siku katika kufikia malengo ya milenia .

Akizungumza hayo katika hafla fupi ya kuzindua maonesho ya picha Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Afya , maendeleo ya Jamii , Jinsia na Watoto , Mkurugenzi wa Tiba Dkt. Margaret Mbando amesema kuwa Tanzania imepiga hatua katika kufikia malengo ya milenia kwa kupunguza Idadi ya vifo kwa watoto wachanga na wakina mama.

“Tumefanikiwa kupunguza Idadi ya vifo kwa watoto wachanga na wakina mama ili kufikia malengo ya milenia kwa upande wa afya kupitia mfumo wa kujiunga na bima ya afya kwa jamii” alisema Dkt. Mbando.

Mbali na hayo Dkt Mbando amesema kuwa amewakaribisha wananchi wote hususani wakazi wa Dar es salaam kuudhuria maonesho hayo yaliyofunguliwa leo yenye kauli mbiu ya “Huduma Bora kwa Afya Bora”yatayofikia kilele mpaka Juni 10 mwaka huu ili kupata ujumbe zaidi kupitia picha yanayofanyika Makumbusho ya Taifa jijini.

Aidha ameipongeza Serikali ya Ujerumani kupitia ubalozi wake kwa kushirikiana vizuri na Serikali ya Tanzania na kukubaliana kupata msaada wa Euro milioni 47 kwa muda wa miaka mitatu ijayo katika kuinua sekta ya Afya.

Kwa upande wa balozi wa Ujerumani Mhe. Egon Kochanke amesema kuwa mchango wa Serikali ya ujerumani kwa sekta ya afya Tanzania utaendelea kuwa sehemu ya mpango wa ushirikiano wa nchi mbili ili kuinua sekta hiyo nchini.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...