1.
: waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia
na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako akiongea na wafanyakazi wa Wizara.
wafanyakazi wa Wizara ya
Elimu Sayansi Teknolojia na Ufundi wakimsikiliza Waziri wa Elimu Profesa Joyce
Ndalichako.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu,
Sayansi, Teknolojia na Ufundi Maimuna Tarishi akimkaribisha Waziri wa Elimu
kuongea na wafanyakazi.
waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako
akiingia katika ukumbi wa Karimjee kuongea na wafanyakazi wa Wizara.
Profesa Ndalichako aliyasema hayo wakati akizungumza na Watumishi wa Wizara hiyo kutoka Makao Makuu katika ukumbi wa Mikutano wa Karimjee ikiwa ni mara ya kwanza kukutana nao tangu alipoteuliwa kuwa Waziri wa Elimu, Sayansi Teknolojia na Ufundi lengo likiwa ni kuwasikiliza lakini pia kujadiliana nao namna bora zaidi ya kuboresha utendaji kazi katika wizara hiyo.
Waziri Ndalichako aliwataka wafanyakazi kufanya kazi kujituma, kutoa huduma bora kwa wakati kwa kuwa ni watumishi wa umma na maana ya mtumishi wa umma ni kuwa na wajibu wa kuwatumikia wananchi ili wapate haki yao kwa wakati kwani haki iliyocheleweshwa ni sawa na haki iliyoptea.
Amewataka watumishi hao kuipende kazi yao, kwa maana mtumishi anayependa kazi yake uifahamu kwa undani wake na inakuwa rahisi kuwatyumika wananchi bila ya kuwa na wasiwasi na kujiamini zaidi .“kila mfanyakazi ni lazima kujivika joho la Wizara kwa maana ya kuijua Wizara vizuri, misingi yake, dira pamoja na sera zinazotuongoza katika utendaji kazi wetu ili tuweze kufikia malengo ya kuinua ubora wa elimu” alisisitza Ndalichako.
Akizungumza kwa niaba ya watumishi Omary Mkali alimshukuru Waziri kwa kukutana na watumishi na kuahidi kufanyia kazi maelekezo yote yaliyotolewa na Waziri ili kuweze kufikia lengo kwa pamoja la kuinua ubora wa Elimu nchini.
No comments:
Post a Comment