Mgakuzi wa Vyakula kutoka Mamlaka a Chakula na Dawa, Dk Itikija Mwanga (kushoto) akitoa maelezo kwa Waziri
wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba na Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu walipotembelea
machinjio hayo, Vingunguti jijini Dar es Salaam .
WIKI
moja baada ya Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kuyafunga machinjio ya
Ng’ombe na Mbuzi Vingunguti jijini Dar es Salaam kwa uchafu na
kusababisha bei ya nyama kupanda, serikali imeitaka Halmashauri ya
Manipaa ya Ilala kufanya marekebisho ya haraka ili uchinjaji uanze mara
moja.
Kaimu
Mkuu wa Idara ya Mifugo katika Manispaa ya Ilala, Msongo Songoro
(kulia) akitoa ufafanuzi juu ya marekebisho yaliyoanza kufanyika
machinjioni hapo wakati Waziri wa
Kilimo,Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba na Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu walipotembelea.
Waziri
wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba akizungumza jambo. Kushoto
ni Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa Vingunguti, Omary
Kumbilamoto.
Moja
ya vitu vilivyo sababisha machinjio hayo kufungwa ni pamoja na mabomba
yote ya karo za kusafishia utombo na nyama kukosa maji. Hii ilieklezwa
na wasimamizi kuwa kila zinapowekwa koki huibiwa.
Mbunge
wa jimbo la Segerea Bona Kaluwa akipita katika moja ya maeneo ya
machinjio hayo ambayo ni machafu na nyama huuzwa humo na kuhatarisha
afya za walaji. Aidha Mbunge huyo alisema kuwa kuna vitendo vichafu
hufanyika machinjioni hapo nyakati za usiku.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
(wapili kulia) akizungumza na Mkaguzi wa Chakula kutoka Mamlaka ya
Chakula na Dawa (TFDA), Dk Itikija Mwanga (kulia) wakati yeye na Waziri
wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba (hayupo pichani)
walipotembelea Machinjio ya Vingunguti Dar es Salaam jana. Kushoto ni
Naibu Meya wa Ilala na Diwani wa Vingunti, Omary Kumbilamoto na wapili
kulia ni Mbunge wa Segerea, Bona Kaluwa
mawaziri hao wakiendelea na ziara yao ya kukagua mazingira ya machinjio hayo.
Hapa
ni sehemu ya kuhifadhia nyama na kuuzwa ambayo nayo imelalamikiwa kuwa
vyuma vyake vuina kutu na pia ni makosa kuuza nyama katika machinjio.
Kutu ilivyo katika vyuma hivyo.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na
Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba wakijadiliana jambo.
No comments:
Post a Comment