March 20
2016 ni siku ambayo Uchaguzi wa marudio Zanzibar utafanyika, zikiwa
zimebaki siku chache kufanywa kwa uchaguzi huo, matukio mbalimbali
yamekuwa yakichukua vichwa vya habari ikiwamo nyumba ya Kamshina wa
polisi kulipuliwa na kitu kinachodhaniwa kuwa ni bomu.
Leo March 17 2016 Chama cha Wananchi CUF wamejitokeza mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es salaam kupitia Naibu katibu Mkuu Magdalena Sakaya
kuitaka Serikali iingilie kati vitendo vinavyofanywa na watu wanaojiita
‘mazombi’ kwa kuwapiga wananchi na wafuasi wa chama hicho, aidha
wamewashutumu polisi kwa kuwashikilia viongozi wa chama hicho bila
sababu…
>>>’Kumekuwa
na vikundi viovu vikiwavamia wafuasi wa CUF na kuwapiga pamoja na
kuwajeruhi, maarufu kwa jina la mazombi jeshi la polisi mpaka leo hii
hawajakamata Zombi hata mmoja na wanasema kwamba hao mazombi hawawajui
na hawapo, lakini cha kushangaza kila tukio baya likitokea Zanzibar
wanasingiziwa wafuasi wa CUF‘:-Magdalena Sakaya
No comments:
Post a Comment